Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Huo msosi wa Haaland ni balaa

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa Man City, Haaland ameripotiwa kuwa na ratiba ya kula mara sita kwa siku na misosi mingine amekuwa akipika mwenyewe, ikiwamo kuchoma nyama kwenye jiko maalumu lililopo kwenye bustani za nyumbani kwake.

MANCHESTER, ENGLAND: WANASEMA hata uwe na shida vipi, usiache kula na hicho ndicho anachokifanya mtambo wa mabao wa Manchester City, Erling Haaland, anayejipongeza kila baada ya mechi kwa kupiga misosi ya nguvu ili kujiweka fiti.

Fowadi huyo wa Man City, Haaland ameripotiwa kuwa na ratiba ya kula mara sita kwa siku na misosi mingine amekuwa akipika mwenyewe, ikiwamo kuchoma nyama kwenye jiko maalumu lililopo kwenye bustani za nyumbani kwake.

Katika posti yake katika mtandao wa Instagram, straika Haaland alionyesha picha ya meza iliyojaa aina tofauti ya vyakula, ikiwa ni sehemu ya misosi yake ambayo amekuwa akila.

Haaland, 25, ambaye amefunga mabao 18 katika michuano yote msimu huu, alionyesha misosi yake anayokula na hilo linatuma taswira ya moja kwa moja ya nguvu zake alizonazo uwanjani.

Swahiba wake, Sander Berge, ambaye ni mchezaji wa Fulham alifichua wamekuwa wakikutana kila Jumapili na kugonga misosi ya maana hasa kwenye mlo wa usiku.

Alisema: “Huwa tunakula vyakula vizuri na kufurahi. Jumapili inakuwa ni ya misosi tofauti. Tumekuwa na muda wa kutosha, naye ni mtu safi na tabia safi, akiwa Mnorwayi mwenzangu.”

Baba yake straika huyo, ambaye ni staa wa zamani wa Leeds United, Alf-Inge Haaland, alisema mwanaye amekuwa akifuata ratiba ya mlo ya supastaa wa Ureno, Cristiano Ronaldo baada ya kumsikia beki wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra alivyotaja vyakula vya mkali huyo.

Baba Haaland alisema: “Nilikuwa na vitu vyangu nilivyofanya kwenye soka. Lakini, Erling anafanya kila kitu, aliondoka nyumbani akiwa na umri wa miaka 16 na tangu wakati huo amekuwa akiendesha mambo yake kwa weledi. Aliwahi kusikia hadithi ya Patrice Evra kuhusu chakula anachokula Ronaldo. Erling anajaribu kuiga kwa sababu anamwona jinsi Ronaldo anavyoendelea kucheza soka la kiwango cha juu hadi sasa, hiyo inaonyesha anafanya sahihi.”