Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Hawa jamaa utawaona Marekani

USA Pict

Muktasari:

  • Fainali hizo zitakazoshirikisha timu 32 zitakazochuana kuwania ubingwa unaotajwa kuwa na zawadi ya pesa ya Pauni 100 milioni, zilianza alfajiri ya kuamkia Jumapili hii, ambapo Al Alhy ilikipiga na Inter Miami.

MIAMI, MAREKANI: FAINALI za Kombe la Dunia la Klabu zimeanza kwa kasi huko Marekani, lakini kivutio kikubwa ni kwa mashabiki wa soka kushuhudia mastaa ambao awali walisahaulika kama bado wanacheza, ila wapo kwenye fainali hizo.

Fainali hizo zitakazoshirikisha timu 32 zitakazochuana kuwania ubingwa unaotajwa kuwa na zawadi ya pesa ya Pauni 100 milioni, zilianza alfajiri ya kuamkia Jumapili hii, ambapo Al Alhy ilikipiga na Inter Miami.

Hii hapa orodha ya mastaa ambao wengi waliwasahau baada ya kutowasikia kwa muda mrefu, lakini wapo kwenye fainali hizo, huku wingi wao ukitosha kutengeneza kikosi pamoja na wachezaji wa akiba.

Kipa: Hugo Lloris (LAFC); Nahodha wa zamani wa Tottenham, sasa akiwa na umri wa miaka 38, yupo kwenye kikosi cha LAFC ambazo kitashiriki fainali hizo, kikipangwa kwenye Kundi D na kitacheza mechi ya kwanza dhidi ya Chelsea.

Beki wa kati: Sergio Ramos (Monterrey); Baada ya kuingoza Real Madrid kwenye michuano minne ya Kombe la Dunia, Ramos sasa anakipiga katika timu ya Mexico ya Monterrey na atakuwapo kwenye fainali hizo za Marekani. Umri wake ni miaka 39 timu yake imepangwa Kundi E sambamba na Inter Milan na River Plate.

Beki wa kati: Thiago Silva (Fluminense); Mashabiki wa PSG na Chelsea wanamfahamu vyema beki huyo wa kati wa Kibrazili na baada ya kuwa kimya sana, kumbe anakipiga Fluminense na umri wake wa sasa ni miaka 40. Silva kwenye fainali za Kombe la Dunia huko Marekani atakuwa na kazi ya kuwakabili Borussia Dortmund.

Beki wa kati: Nicolas Otamendi (Benfica); Bingwa mara mbili wa Ligi Kuu England akiwa na Man City, Otamendi hajabeba ubingwa mwingine tangu alipoondoka Etihad. Huu ni msimu wake wa tano huko Benfica na kwenye umri wa miaka 37 bado hajatundika daruga na atakuwapo kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu kuchuana na Bayern.

Wing-Back wa kulia: Joao Cancelo (Al-Hilal); Kuna wakati alitambulika kama moja ya mabeki wa pembeni bora kabisa duniani, akitamba kwenye timu za Inter Milan, Juventus, Man City, Bayern Munich na Barcelona. Kwa sasa yupo Al-Hilal ya Saudi Arabia na atakuwapo huko Marekani, timu yake ikipangwa Kundi H sambamba na Real Madrid.

Kiungo wa kati: Ander Herrara (Boca Juniors); Ni miaka sita tangu Herrera, 35, alipoondoka Old Trafford alipokuwa akitamba na jezi ya Manchester United. Baada ya kuondoka PSG na kisha Athletic Bilbao, wengi walidhani Herrera amepotea, lakini kumbe yupo Boca Juniors na atakipiga kwenye Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani.

Kiungo wa kati: Ruben Neves (Al-Hilal); Hakuchukuliwa na timu nyingine ya Ligi Kuu England baada ya kuondoka Wolves alikocheza kwa ubora mkubwa. Katika umri wa miaka 28, Neves amekuwa kimya, lakini anakipiga huko Al-Hilal na atakuwapo kwenye fainali za Marekani.

Wing-Back wa kushoto: Alex Telles (Botafogo); Baada ya kuachana na Manchester United, Telles, 32, aliondoka na kwenda kuonyesha uwezo wake wa mguu wa kushoto. Baada ya kushinda mataji huko Galatasaray na Porto, hakuwa poa Old Trafford alikoondoka kwenda Sevilla, Al-Nassr na Botafogo, itakayokuwapo Marekani.

Kiungo mshambuliaji: Angel Di Maria (Benfica); Winga matata aliyetamba Real Madrid, Man United na PSG. Staa huyo atarudi kwenye klabu ya kwao huko Rosario Central dirisha hili, lakini kwa sasa atakuwa kwenye kikosi cha Benfica wakati wa fainali hizo za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani.

Mshambuliaji: Edinson Cavani (Boca Juniors); Staa mwingine wa zamani wa Man United na PSG, mbaye alikuwa kimya sana ikidhaniwa kwamba ametoweka kwenye soka, kumbe bado yupo na atakuwapo kwenye fainali za Kombe la Dunia akiitumia Boca Juniors.

Mshambuliaji: Olivier Giroud (LAFC); Utashangaa, lakini ndiyo hivyo, Giroud bado anakipiga na sasa yupo kwenye kikosi cha LAFC kitakachoshiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani.