Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Eti Man United kuna laana

LAANA Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 22 alipitia misimu miwili migumu akiwa Old Trafford baada ya kujiunga kwa dau la Pauni 72 milioni akitokea Atalanta.

MANCHESTER, ENGLAND: MASHABIKI wa Manchester United wanaamini klabu yao “imerogwa” baada ya kuona kiwango ambacho mshambuliaji wao Rasmus Hojlund alikionyesha katika mechi yake ya kwanza akiwa na Napoli kwa mkopo msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 22 alipitia misimu miwili migumu akiwa Old Trafford baada ya kujiunga kwa dau la Pauni 72 milioni akitokea Atalanta.

Aliondoka mwezi uliopita, akirudi Italia kujiunga na mabingwa wa Serie A, Napoli kwa mkopo wa msimu mmoja.

Awali, Hojlund alikuwa akitajwa kama mshambuliaji wa kasi na atakayekwenda  kuisaidia sana Man United baada ya kujiunga nayo.

Hata hivyo, katika misimu miwili iliyopita akiwa na mashetani wekundu, alishindwa kufikia malengo na matarajio ya mashabiki wengi.

Uhamisho wake wa kurejea Serie A ulifanyika mara tu baada ya Man United kumsajili Benjamin Sesko kutoka RB Leipzig kwa Pauni 74 milioni.

Mkataba wake wa mkopo na Napoli una kipengele cha kununuliwa moja kwa moja kwa dau la Pauni 38 milioni ambacho kitatumika ikiwa tu Napoli itapata nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Hojlund alifunga bao moja katika mchezo dhidi ya Fiorentina ambao ulimalizika kwa Napoli kushinda mabao 3-1.

Bao hilo lilikuwa la kwanza la mchezo wa ligi kwa Hojlund tangu Aprili mwaka huu licha ya kwamba aliwahi kufunga Mei katika Europa League na pia aliifungia Denmark bao katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Ugiriki wiki iliyopita.

Baada ya mechi hiyo kupitia mitandao ya kijamii mashabiki wengi walitoa maoni yao kwamba huenda timu yao itakuwa imerogwa na kuweka wazi kwamba mchezaji huyo hakuwa na kiwango kibovu.

Shabiki mmoja aliandika: “Goli la kwanza tu kwenye mchezo wetu wa kwanza, Man United wamelogwa."

Wa pili akasema: "Hojlund kafunga mechi ya kwanza? Tumelaaniwa kweli."

Wa tatu akaongeza: "Kweli tumerogwa."

Mwingine akahoji: "Basi tatizo ni Manchester United yenyewe?"

Wa tano akaandika: "Nimeamini kabisa Man United ndio tuna shida."

Napoli waliongeza bao la tatu kupitia Sam Beukema katika dakika ya 51, huku Fiorentina ikifunga bao la kufutia machozi kupitia kwa Luca Ranieri.