Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Enrique analeta dharau kwa Liverpool

Muktasari:

  • Miamba miwili, PSG na Liverpool inakutana kwenye hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo kipute cha kwanza kitapigwa Parc des Princes, Jumatano, Machi 5.

PARIS, UFARANSA: KOCHA wa Paris Saint-Germain, Luis Enrique amesema Liverpool na Lille “zinafanana” huku akidai ushindi ilioupata timu yake dhidi ya Lille wa mabao 4-1 Jumamosi iliyopita ilikuwa ni mazoezi tu.

Miamba miwili, PSG na Liverpool inakutana kwenye hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo kipute cha kwanza kitapigwa Parc des Princes, Jumatano, Machi 5.

Liverpool iliongoza msimamo wa Ligi Kuu England kwenye hatua ya makundi, wakati PSG ilihitaji kucheza mechi ya mchujo dhidi ya Wafaransa wenzao, Brest kutinga kwenye mtoano.

Lille pia ipo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo ilipoteza mechi mbili tu kwenye hatua ya makundi, ambapo moja ya mechi hizo ni ile iliyocheza na Liverpool.

Kwenye Ligue 1, Lille ipo kwenye nafasi ya tano, ikiwa imeshinda mechi 11 na kupoteza tano katika mechi ilizocheza hadi sasa. Ipo pointi 21 nyuma ya PSG, ambao wapo kileleni, wakati Liverpool yenyewe pia ipo kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, ikiongoza msimamo kwa tofauti ya pointi 13 dhidi ya Arsenal inayoshika nafasi ya pili, lakini Enrique anawaona wanacheza staili inayofanana na Lille.

Alisema: “Hatutakwenda kubadilika sana, mechi hii ilikuwa majaribio, Liverpool na Lille wana vitu vinavyofanana, tutaweka kwenye presha ya kuwazuia wasicheze kutokea nyuma, wachezaji mipira mirefu. Itakuwa tofauti, itakuwa na upinzani, lakini tupo kwenye kipindi kizuri msimu huu. Tutacheza na timu bora Ulaya, ina viwango, lakini haipo kwenye akili yetu kwenda kukaba, tutajaribu kuwashambulia.€

“Naifahamu vyema Liverpool na haina ubishi ni timu bora Ulaya na kwenye ishu ya matokeo na kucheza. Itakuwa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, tutajaribu kutumia silaha zetu zote.”€

PSG huu ni msimu wa kwanza kwenye Ligi Kuu Ufaransa bila huduma ya Kylian Mbappe ambaye ametimkia Real Madrid.