Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diarra naye nje Afcon, Mali yachapwa na Senegal

MALI Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa Everton alikuwa mahali sahihi kuunganisha mpira kutoka umbali wa mita tano tu baada ya kipa wa Mali, Djigui Diarra, kushindwa kuudaka mpira wa chini uliopigwa kutoka upande wa kulia na Krepin Diatta.

TANGIER, MOROCCO: BAO la Iliman Ndiaye katika kipindi cha kwanza lilitosha kuipa Senegal ushindi dhidi ya Mali iliyokuwa na wachezaji 10 na hivyo kutinga nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 baada ya kushinda 1-0 katika mechi iliyofanyika uwanjani Grand Stade de Tanger.

Mshambuliaji huyo wa Everton alikuwa mahali sahihi kuunganisha mpira kutoka umbali wa mita tano tu baada ya kipa wa Mali, Djigui Diarra, kushindwa kuudaka mpira wa chini uliopigwa kutoka upande wa kulia na Krepin Diatta.

Diarra aliokoa shuti la El Hadji Malick Diouf na kuugonga mpira juu ya mwamba wa lango katika muda wa nyongeza wa kipindi cha kwanza, kabla ya nahodha wa Eagles na kiungo wa Tottenham, Yves Bissouma, kutolewa nje kwa nyekundu baada ya kuonyesha kadi ya pili ya njano.

Katika kipindi cha pili katika mchezo huo uliochezwa huko Tangier, kipa wa Senegal Edouard Mendy alimzuia Abdoulaye Diaby kabla ya Diarra kuokoa mashuti ya Sadio Mane na Pathe Ciss.

Ciss alikosa nafasi nyingine kwa mabingwa wa 2021 baada ya kupiga shuti moja kwa moja kwa Diarra kufuatia kosa la ulinzi, na baadaye kipa wa Eagles aliokoa kwa kuugusa mpira wa mkwaju wa voli uliopigwa na Lassine Camara na kuugongesha kwenye nguzo ya kulia katika muda wa nyongeza.

Mali inaondoka kwenye mashindano bila kushinda mechi hata moja huku ukosefu wao wa nidhamu ukiwagharimu, wakimpoteza mchezaji kwa kadi nyekundu katika mechi yao ya tatu mfululizo nchini Morocco.

Eagles watakuwa na furaha kumaliza kushughulika na mwamuzi Abongile Tom, ambaye pia alisimamia mechi yao ya hatua ya 16 bora dhidi ya Tunisia na alimpa Woyo Coulibaly kadi nyekundu ya moja kwa moja.

Senegal itawajua wapinzani wao wa nusu fainali siku ya Jumamosi, wakati mabingwa wa rekodi mara saba, Misri watakapokutana na mabingwa watetezi Ivory Coast mjini Agadir.