Dea Gea ashinda tuzo EPL

MANCHESTER, ENGLAND.KIPA wa Manchester United, David De Gea atapewa atatunukiwa tuzo ya Golden Glove ya Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuibuka kuwa kipa ambaye hajaruhusu nyavu zake kutikiswa mara 16.

De Gea, amemzidi kipa wa Liverpool, Allison ambaye ameshika nafasi ya pili, kwani hajaruhusu nyavu zake kutikiswa mara 14 msimu huu huku akiwa amebakiza mechi moja baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Aston Villa.
Kipa wa Newcastle, Nick Pope na kipa wa Arsenal, Aaron Ramsdale, wote hawajaruhusu nyavu zao kutikiswa mara 13, De Gea akiwazidi.

De Gea atapewa tuzo hiyo ya Ligi Kuu England kwa mara ya pili, kwani Mhispania huyo mara ya mwisho kubeba ilikuwa msimu wa 2017-2018.

De Gea, 32, amekuwa akikosolewa mara kwa mara lakini ameonyesha kiwango bora na kutoruhusu timu yake kutofungwa katika nusu ya mechi za ligi msimu huu.
Hata hivyo hatima ya De Gea ndani ya viunga vya Old Trafford bado haijaeleweka, kwani kipa huyo huenda akapewa ofa ya kusaini mkataba mpya lakini atakatwa mshahara wake anaolipwa Pauni 375,000.

Kipa huyo wa kimataifa wa Hispania amefanikiwa kubeba mataji mbalimbali na Man United kama Ligi Kuu, Carabao, FA na Europa katika historia ya soka lake. De Gea amecheza mechi 540 na amekuwa miongoni katika orodha makipa bora Ligi Kuu England wa muda wote .

Kocha Erik ten Hag aliweka wazi sababu ya kiwango cha De Gea kushuka msimu huu na haikuhusiana na masuala yake ya mkataba: "Kwani ndio sababu? hapana sidhani kwasababu De Gea ana uzoefu, naweza kufikiria sababau kibao lakini hiyo sio sababu, kama mchezaji mkubwa kuna wakati utapitia kipindi kigumu tu"