Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Bruyne, Napoli kitu kimeeleweka

BRUYNE Pict

Muktasari:

  • De Bruyne anaachana na Manchester City akiwa mchezaji huru baada ya miamba hiyo ya Ligi Kuu England kuamua kutomuongezea mkataba staa huyo wa Kibelgiji.

NAPLES, ITALIA: KIUNGO Kevin De Bruyne anajiandaa kujiunga na Napoli kwa dili la mkataba wa miaka miwili baada ya kufikia makubaliano na mabingwa hao wa Italia.

De Bruyne anaachana na Manchester City akiwa mchezaji huru baada ya miamba hiyo ya Ligi Kuu England kuamua kutomuongezea mkataba staa huyo wa Kibelgiji.

Ilithibitishwa tangu Aprili mwaka huu kwamba De Bruyne ataachana na Man City mwisho wa msimu. Jambo hilo lilimfanya nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 kuwa na muda wa kutosha wa kufanya uamuzi wa kitu  cha kufanya huku kukiwa na klabu nyingine za Ligi Kuu England zikihitaji saini yake pamoja na miamba ya soka ya ligi ya Marekani, MLS.

Lakini, Napoli iliwahi mbele haraka kumpa ofa tamu na sasa yupo kwenye hatua nzuri ya kujiunga huko Naples. Baada ya mechi ya kimataifa ambapo alifunga bao la ushindi Ubelgiji ilipoichapa Wales 4-3, Jumatatu iliyopita, De Bruyne alifichua mambo yake yameshakaa vizuri.

Ripoti zinafichua kwamba amefikia makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka miwili  Napoli, huku kukiwa na kipengele cha kuongeza zaidi kama mambo yatakuwa mazuri. De Bruyne atasafiri kwenda Naples, Alhamisi kwa ajili ya kufanya vipimo na kinachoelezwa ni kwamba tayari ameshanunua nyumba ya familia yake, kwa mujibu wa rais wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis.

Rais huyo alisema mwezi uliopita: “Naamini ameshanunua nyumba nzuri. Asubuhi hii nilizungumza naye kwa njia ya video, yeye mke wake pamoja na kijana wao wa miaka 9, ilikuwa picha nzuri sana.” Rekodi za De Bruyne huko Man City amefunga mabao 108 na asisti 177 katika mechi 422, huku akishinda mataji 16 ikiwamo sita ya Ligi Kuu England na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Atakwenda Napoli kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Antonio Conte, huku kikimsaka pia winga wa Manchester United, Alejandro Garnacho. De Druyne atakutana na wakali wa zamani wa Ligi Kuu England ambao ni Mbelgiji mwenzake Romelu Lukaku, Scott McTominay na Billy Gilmour.