Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Bruyne moja haikai, mbili haikai

KDB Pict

Muktasari:

  • De Bruyne ataondoka Man City wakati mkataba wake utakapofika tamati Juni 30 - ikiwa ni wiki mbili na nusu baada ya kuanza kwa michuano hiyo ya Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani.

MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO fundi wa mpira, Kevin De Bruyne ameripotiwa kwamba bado hajafanya uamuzi wa mwisho kama atakwenda kuichezea Manchester City kwenye michuano ijayo ya Kombe la Dunia la Klabu mwezi ujao.

De Bruyne ataondoka Man City wakati mkataba wake utakapofika tamati Juni 30 - ikiwa ni wiki mbili na nusu baada ya kuanza kwa michuano hiyo ya Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani.

Lakini, kiungo huyo Mbelgiji, ambaye alishinda mataji 19 katika muda wake alioutumikia Man City, alisema bado hana uhakika kama atakwenda Marekani, kwa kuwa mkataba wake utafika mwisho katikati ya michuano hiyo, aliposema: "Haingii akilini, lakini hilo linatokea unapojaribu michuano mipya katika sintofahamu ya mambo ya kimkataba. Lazima nijijali, unadhani nikienda kuumia kwenye Kombe la Dunia la Klabu, nitafanya nini baada ya hapo? Hakuna mtu atajali. Hivyo, kuna uwezekano mkubwa nisiende kucheza, lakini bado sijapata uamuzi wa mwisho.

"Mimi ni mchezaji tu, sio mtunga sheria au kanuni, sina cha kufanya juu ya hilo. Lakini, mwisho ya yote ni lazima nijijali mwenyewe, ambao ni uamuzi wa kawaida tu."

De Bruyne amethibitisha kuwa kwenye mazungumzo na klabu nyingine, lakini bado hajafanya uamuzi wa mwisho ni wapi atakwenda kucheza msimu ujao.

"Nataka kucheza soka zuri kwa uamuzi wowote nitakaofanya," alisema De Bruyne na kuongeza: "Nafahamu mnajaribu kuotea ni wapi nitakwenda, lakini nitafanya uamuzi wangu na hilo litafahamika."

De Bruyne alitangaza kwamba ataachana na miamba hiyo ya Etihad mwishoni mwa msimu huu, lakini kocha Pep Guardiola atapenda kuwa naye kwenye Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani.