Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea v PSG kombe la Dunia fainali ya pesa

Muktasari:

  • Vijana wa Enzo Maresca, Chelsea waliiondoa Fluminense ya Brazil kwa mabao 2-0 wakati matajiri wa Jiji la Paris, PSG wakiinyoosha Real Madrid kwa  kipigo cha 4-0.

NEW YORK, MAREKANI: CHELSEA na PSG zimeonyesha kiu yao ya kubeba ubingwa wa fainali za Kombe la Dunia kwa Klabu baada ya kutinga fainali kibabe baada ya kushinda mechi za nusu fainali katika michuano inayoendelea huko Marekani.

Vijana wa Enzo Maresca, Chelsea waliiondoa Fluminense ya Brazil kwa mabao 2-0 wakati matajiri wa Jiji la Paris, PSG wakiinyoosha Real Madrid kwa  kipigo cha 4-0.

Baada ya kufika hatua hiyo, timu zote mbili zimejikusanyia mamilioni ya pesa kama zawadi kwa viwango vyao katika michuano hii.

Kwa mujibu wa takwimu hadi sasa timu hizo kila moja imekunja dola 88.43 milioni.

Vilevile wapinzani wao Fluminense imeondoka na dola 60.83 milioni na Real Madrid dola 59.43 milioni.

Hata hivyo, kwa upande wa Chelsea na PSG pesa walizopata zinaweza kuongeza kufikia dola 130 milioni ikitegemea na matokeo ya fainali, lakini zote haziwezi kufikia dola 155 milioni hata ikichukua taji hilo kwa sababu tayari ilipoteza mechi moja kati hatua ya makundi, lakini inaweza kufikia dola 130 milioni.

Kiasi hicho cha dola 155 milioni ni mjumuisho ikiwa timu itashinda mechi zote za hatua ya makundi ambapo kila ushindi una zawadi ya dola 2 milioni, pia ikashinda hatua zinazofuatia hadi fainali.

Vilevile ukiondoa pesa za ushindi katika mechi, dola 155 milioni ni mjumuisho wa pesa ambazo timu zimepewa kwa ushiriki wao ambapo timu za Ulaya ndizo zimekunja pesa nyingi zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa kila timu inayotoka Ulaya iliyocheza michuano hii imepata kati ya dola 12 milioni hadi dola 38 milioni ambazo zikiunganishwa na zile za ushindi, timu hujikuta zinapata kiasi hicho cha dola 130 milioni hadi dola 155 milioni.

Mchezo huu wa fainali unatarajiwa kupigwa Jumapili kwenye Uwanja wa MetLife, huko East Rutherford kuanzia saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Tiketi za mechi hii zinaanzia dola 265 kwa baadhi ya tovuti zinazouza lakini kuna tiketi za bei ghali zaidi ambazo zinafikia dola 1500.

Kumekuwa pia na ulanguzi wa tiketi kwa watu wanaonunua kisha kuziuza kwa mashabiki wengine ambapo ripoti zinaeleza kuna watu wanauza tiketi hizo kwa zaidi ya dola 2000.

Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kuhudhuria fainali hiyo ya Jumapili itakayohitimisha michuano hiyo. kwa mwaka 2025.