Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea kiroho safi kwa Enzo Fernandez

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mkataba wa sasa wa Enzo unatarajiwa kumalizika mwaka 2032 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 46 za michuano yote na kufunga mabao 12. Hivi karibuni staa huyu aliingia katika matatizo baada ya kutamka kauli zilizoashiria kuwa anataka kuondoka mwisho wa msimu huu kujiunga na Real Madrid.

CHELSEA inaweza kumuweka sokoni kiungo wake wa kimataifa wa Argentina, Enzo Fernandez, 25, katika dirisha la majira ya kiangazi ikiwa itashindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao.

Nyota huyo tayari anahusishwa na Real Madrid ambayo inaendelea kumfuatilia kwa karibu kwa muda sasa.

Mkataba wa sasa wa Enzo unatarajiwa kumalizika mwaka 2032 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 46 za michuano yote na kufunga mabao 12. Hivi karibuni staa huyu aliingia katika matatizo baada ya kutamka kauli zilizoashiria kuwa anataka kuondoka mwisho wa msimu huu kujiunga na Real Madrid.

Hali hiyo ilisababisha asimamishwe takribani mechi mbili na uongozi wa Chelsea ambao sasa unadaiwa kuwa unafikiria kuachana naye mwisho wa msimu huu ikiwa tu Madrid inayodaiwa kumhitaji itawasilisha ofa sahihi.

Wakala wa fundi huyu anaripotiwa kuwa tayari ameshaanza mazungumzo na Madrid, kujadili masuala ya maslahi binafsi.


Andy Robertson

TOTTENHAM Hotspur inaonekana kuwa kinara katika mbio za kumsajili beki wa kushoto wa Liverpool na timu ya taifa ya Scotland, Andy Robertson, 32, kama mchezaji huru katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hata hivyo, dili hilo litategemea hatma ya Spurs msimu huu, ikiwa itabakia katika Ligi Kuu England au itashuka daraja.

Robertson, ambaye ni miongoni mwa mabeki bora wa kushoto katika miaka ya hivi karibuni, ana uzoefu mkubwa wa Ligi Kuu England na michuano ya Ulaya, jambo linalomfanya kuwa chaguo muhimu kwa Tottenham Hotspur.


Morten Hjulmand

MANCHESTER City imeripotiwa kufanya mazungumzo yasiyo rasmi na Sporting Lisbon kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo mkabaji wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Denmark, Morten Hjulmand, 26, katika dirisha lijalo la usajili.

Hjulmand ameibuka kuwa mmoja wa viungo bora wa ulinzi katika ligi ya Ureno msimu huu, hali iliyovutia pia vigogo wengine wa Ulaya akiwemo Manchester United na Juventus.

Manchester City inaonekana kutafuta mbadala au kuongeza nguvu katika eneo la kiungo ambalo msimu huu linaonekana kuwa na upungufu.


Ederson

KIUNGO wa Atalanta, Ederson Jose dos Santos Lourenco da Silva maarufu Ederson, 26, ameripotiwa kukataa ofa kutoka kwa klabu kadhaa za Ligi Kuu England ikiwemo Arsenal, Manchester United na Newcastle United.

Nyota huyo wa Brazil anadaiwa kuwa ana nia ya kujiunga na Atletico Madrid, ambayo inaonekana kuwa ndiyo chaguo lake kuu kwa sasa.

Hata hivyo, uamuzi huenda ukabadilika kwa sababu timu hizo za England zinafikiria kuwasilisha ofa nono kwenda Atalanta ili kumsajili.


Morgan Rogers

MSHAMBULIAJI wa Aston Villa na timu ya taifa ya England, Morgan Rogers, 23, yupo katika rada za timu kubwa barani ambazo ni pamoja na Manchester United, Arsenal, Paris Saint-Germain na Chelsea.

Rogers ameonyesha kiwango cha kuvutia msimu huu akiwa na Aston Villa, jambo lililoongeza thamani yake sokoni na kumfanya kuwa mmoja wa washambuliaji wanaowindwa sana.

Kutokana na idadi ya klabu zinazomtaka, bei ya staa huyu inaonekana kuwa huenda ikapanda kufikia Pauni 70 milioni.


Anthony Gordon

ARSENAL inaendelea kufanya harakati za kimya kimya kuhusu hali ya winga wa Newcastle United na England, Anthony Gordon, 25, ambaye inataka kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi.

Ripoti zinaeleza kuwa Arsenal inaweza kutoa takribani Pauni 80 milioni kama ofa ya ada ya uhamisho wa fundi huyu, kiasi ambacho kinaonekana kuwa kidogo ikilinganishwa na kile ambacho Newcastle inakihitaji.

Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Newcastle wanahitaji takribani Pauni 100 milioni ili kumuuza staa huyo.


Benjamin Nygren

CELITIC ipo tayari kumuuza winga wao wa kimataifa wa Sweden, Benjamin Nygren, 24, katika dirisha la majira ya kiangazi lakini kwa klabu itakayokuwa tayari kutoa ofa itakayoanzia takribani Pauni 26 milioni.

Nyota huyo anavutiwa na klabu kadhaa, huku Tottenham Hotspur ikionekana kuwa ndiyo inaongoza katika vita ya kuiwania saini yake.

Mbali ya Spurs, huduma ya fundi huyu pia inahitajika na Brighton, AFC Bournemouth na Valencia.


Neymar Jr

TIMU ya FC Cincinnati ya Marekani imeanza kufanya mazungumzo kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Santos,

Mbrazili Neymar Jr, 34, baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia. Ripoti zinaeleza kuwa tayari mazungumzo ya awali yamefikia hatua nzuri na Cincinnati inamwangalia Neymar kama mchezaji atakayesaidia sana timu yao katika upande wa mvuto na kibiashara.

Hata hivyo, Neymar amekuwa katika nyakati ngumu za majeraha ya mara kwa mara kwa mwaka wa tatu sasa, hali inayosababisha asionyeshe kiwango chake.