Casemiro pigo kwa Ten Hag

New Content Item (1)
New Content Item (1)

MANCHESTER, ENGLAND. MCHAMBUZI wa soka Jamie Redknapp amesema Manchester United imepata pigo kutokana na adhabu aliyopewa kiungo wa timu hiyo, Casemiro.
Staa huyo wa kimataifa wa Brazil, ataikosa mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal, utakaochezwa kesho kutwa uwanjani Emirates.

Casemiro amefikisha jumla ya kadi za njano tano msimu huu, baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Crystal Palace, Wilfried Zaha dakika ya 80 ya mtanange wa Ligi Kuu England, uliyochezwa juzi usiku kwenye Uwanja wa Selhurst Park. 

Man United ilipotez pointi tatu muhimu katika dakika za mwisho na kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Crystal Palace, lakini ishu kubwa pigo alilolipata Kocha Erik ten Hag.

Casemiro aliyesajiliwa kwa dau la Pauni 70 milioni ana mchango mkubwa tangu alipotua Old Trafford akitokea Santiago Bernabeu na kupewa sifa na mashabiki wa Mashetani Wekundu.

Lakini mchambuzi na kiungo huyo aliyewahi kukipiga Liverpool na Tottenham, anaamini Casemiro angekuwa mhimili mkubwa eneo la kati katika mchezo huo muhimu dhidi ya Arsenal.

"Mbaya sana kwa Man United hususan baada ya kupoteza pointi dhidi ya Crystal Palace, tuliongea na Casemiro kabla ya mechi na kumsihi acheze kwa makini asipewe kadi, muhimu sana kwa sababu Man United inamuhitaji, baada ya Casemiro kupewa kadi, timu nzima iliathirika kutokana na umuhimu wa Mbrazili huyo," alisema Redknapp.

Wakati huohuo Kocha Ten Hag alizungumzia kuhusu kadi ya Casemiro baada ya mechi huku akisikita kutokana na kuelewa mchango wa Mbrazili huyo.

"Mechi iliyopita tulimfunga Arsenal bila ya Casemiro, safari hii tunacheza kwa mara nyingine bila ya uwepo wake," alisema Ten Hag.

Naye kipa wa Man United, David de Gea alisikitia akidai: "Kumkosa Casemiro kwenye mechi hiyo ni pigo kubwa sana kwao, nashangaa kwa nini wengine tumecheza katikati ya wiki, lakini timu nyingine hazikucheza inashangaza sana."