Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick atofautiana na Ten Hag, Amorim

CARRICK Pict

Muktasari:

  • Wachezaji wa Man United sasa wanapewa siku ya mapumziko siku moja baada ya mechi, hatua ambayo ni tofauti na utaratibu wa enzi za Erik ten Hag na Ruben Amorim.

MANCHESTER, ENGLAND: MICHAEL Carrick amefanya mabadiliko katika ratiba ya mazoezi ya kila wiki Manchester United.

Wachezaji wa Man United sasa wanapewa siku ya mapumziko siku moja baada ya mechi, hatua ambayo ni tofauti na utaratibu wa enzi za Erik ten Hag na Ruben Amorim.

Ten Hag na Amorim walisisitiza kuwepo kwa siku za kurejesha nguvu mara tu baada ya mechi, huku wachezaji ambao hawakucheza angalau dakika 45 wakifanyishwa mazoezi kamili.

Hata hivyo, Carrick ameamua kuwapa wachezaji wa Man United mapumziko siku inayofuata baada ya mechi na vipindi vya kurejesha nguvu hufanyika siku ambayo wachezaji wanaripoti tena katika kituo cha mazoezi cha Carrington. Carrick tayari ameanza kuonyesha mamlaka yake kama kocha mkuu, akipunguza muda wa siku za mazoezi, lakini akiongeza kiwango cha ukali na kasi ya mazoezi.

Kumekuwa na msisitizo zaidi mazoezi binafsi kwa wachezaji maalumu, huku mabeki wa zamani Jonathan Woodgate na Jonny Evans wakifanya kazi kuwanoa mabeki wa kati kuboresha mbinu kwenye ukabaji. Man United pia wanafika uwanjani Old Trafford kwa kuchelewa zaidi siku za mechi, ilhali chini ya Ten Hag walikuwa wakifika takribani saa nne kabla ya mchezo. Ten Hag alikuwa kocha wa kwanza wa Man United kuchukulia siku za kurejesha nguvu kwa uzito, na Amorim aliendeleza utaratibu huo.

Man United karibu kila mara walikuwa na mapumziko siku ya Jumanne msimu huu kutokana na ratiba yao haba ya michezo ya katikati ya wiki, lakini walifanya mazoezi Jumanne wiki hii. Makocha wa zamani wa Man United, David Moyes na Louis van Gaal, walikuwa na haki ya kuwaita wachezaji kufanya mazoezi hata siku za mapumziko endapo timu ingepata matokeo mabaya.

Hata hivyo, Jose Mourinho alihakikisha kila mara kuwa wachezaji wake wa Man United wanakuwa na siku za mapumziko zilizopangwa, bila kujali matokeo ya mechi iliyotangulia. Mabadiliko haya yanamaanisha kuwa wachezaji wa Man United watapata mapumziko Jumapili hii.