Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bundi bado ainyemelea Chelsea

Muktasari:

  • Blues inakabiliwa na adhabu kulipa faini ya Pauni 10.75 milioni pamoja na kufungiwa kusajili kwa mwaka mmoja kutokana na kuvunja sheria za Ligi Kuu England zinazohusu taarifa za kifedha, uwekezaji wa watu na maendeleo ya vijana.

LONDON, ENGLAND: CHELESEA inatarajiwa kukabiliana na adhabu zaidi kutoka mamlaka za soka za England kutokana na uchunguzi unaofanywa na chama cha Soka England (FA).

Blues inakabiliwa na adhabu kulipa faini ya Pauni 10.75 milioni pamoja na kufungiwa kusajili kwa mwaka mmoja kutokana na kuvunja sheria za Ligi Kuu England zinazohusu taarifa za kifedha, uwekezaji wa watu na maendeleo ya vijana.

Hata hivyo, licha ya kukubali kutekeleza adhabu hizo, kumeibuka mapya na adhabu ya kutokusajili imeongezeka kwa mwaka mwingine mmoja. Pia kuna adhabu ya kutokusajili katika kikosi cha timu ya vijana kwa miezi tisa ambavyo vyote vimeanza mara moja.

Utoaji wa adhabu hiyo ulizingatia pia uwasilishwaji wa ripoti ya uvunjaji wa sheria iliyotolewa na wamiliki wa timu hiyo, Todd Boehly na kampuni ya Clearlake Capital na ndiyo iliyoamua ukali wa adhabu.

Hata hivyo, FA imeanzisha uchunguzi wa adhabu tofauti inayohusu uvunjaji wa sheria zinazofanana.

Tayari mashtaka 74 yamewasishwa dhidi ya klabu hiyo ambayo yanaweza kusababisha adhabu zaidi iwapo itatiwa hatiani katika siku chache zijazo.

Mtaalamu wa masuala ya fedha katika soka, Kieran Maguire aliiambia talkSPORT: “Hili linahusu malipo kwa mawakala na wawtu wengine ikiwa ni kama aina fulani ya motisha ili kuwahamasisha wachezaji kujiunga na Chelsea.

“Hili lilitokea hasa enzi za Roman Abramovich na wachezaji waliohusika walitajwa... hata hivyo, hakujakuwa na kosa lolote kwa wachezaji. Wao walitakiwa tu kusaini fomu na walitaka kujiunga na Chelsea. Lakini wachezaji kama Eden Hazard, Willian na Samuel Eto’o wameshutumiwa.

“Hili ni jaribio la kuwahamasisha wengine ili kuwahimiza wateja au wawakilishi wao kuruhusu wachezaji kujiunga na klabu hiyo. Na malipo hayo yalifanywa kutokana na mikataba na akaunti zisizo wazi. Pia, kutokana na ukweli Abramovich alitumia kampuni zilizopo British Virgin Islands na Cayman Islands, mara nyingi ni vigumu kufuatilia malipo hayo.

“Hata hivyo, hakuna tuhuma za udanganyifu. Lakini kulikuwa na karatasi nyingi ambazo hazikushirikiana vizuri.”

Habari za mashtaka hayo zilivuja Septemba na uchunguzi unatarajiwa kuhitimishwa hivi karibuni na licha ya uwezekano wa adhabu kubwa zaidi, talkSPORT inaelewa FA ina mpango wa kufuata hatua ya Ligi Kuu England kwa kutoa faini kubwa kwa klabu.

Kwa sasa, Chelsea haitapoteza pointi kutokana na mashtaka hayo 74 na Machi 2025, talkSPORT iliripoti klabu hiyo ilikuwa inajadili makubaliano ya kifedha na Ligi Kuu England kutokana na uvunjaji wa sheria.

Chelsea walidai hawapaswi kupoteza pointi kwani Abramovich sio mmiliki tena na walijitolea na kushirikiana na mamlaka za ligi, kama walivyofanya na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), kabla ya kulipa Pauni 8 milioni kwa suala la aina hiyo mwaka 2023.

Maguire alisema: “Ndiyo, Chelsea watashangilia nifaini tu badala ya kupoteza pointi. Hii inaonyesha faida ya klabu kutoa ripoti. Wakati Clearlake Capital waliponunua klabu (2022), hili lilikuwa jambo moja walilogundua wakati wa uchunguzi.

“Kwa hivyo, Chelsea wamekuwa na uhakika tangu mwanzo itakuwa adhabu ya faini tu, kutokana na Clearlake kuhifadhi Pauni 150 milioni kutokana na manunuzi ya klabu na hivyo kupigwa faini hiyo ya Pauni 10 milioni. Pia, ishu ya kufungiwa usajili walishajua itatokea wakiamini hawakufanya makosa lakini wanaona hakutakuwa na tatizo kutekeleza adhabu hiyo.”