Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bruno, Mainoo kuikosa Newcastle

Muktasari:

  • Hata hivyo, Amorim alisema Mainoo anaweza kurejea mapema zaidi tofauti na ilivyo kwa Bruno ambaye atakaa nje kwa muda.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amesema hatarajii kuona Bruno Fernandes wala Kobbie Mainoo wakicheza mechi ya leo ya Ligi Kuu England ya Boxing Day dhidi ya Newcastle kutokana na majeraha yanayowasumbua.

Hata hivyo, Amorim alisema Mainoo anaweza kurejea mapema zaidi tofauti na ilivyo kwa Bruno ambaye atakaa nje kwa muda.

Fernandes aliumia kipindi cha kwanza cha mechi dhidi ya Aston Villa mwishoni mwa wiki iliyopita na alishindwa kurejea uwanjani kipindi cha pili baada ya kwenda mapumziko.

Mainoo alipata majeraha mazoezini siku moja kabla ya mchezo wa Villa, lakini halionekani kubwa sana, hivyo yuko karibu kurejea.

“Hapana, sioni wakirejea kwenye mechi dhidi ya Newcastle, wanaendelea vizuri. Sidhani kama watakaa kwa muda mrefu nje na Kobbie atarejea haraka zaidi kuliko Bruno,” alisema Amorim.

Man United itavaana na Manchester City kwenye dabi Januari, 17 mwakani lakini bado haijajulikana kama nahodha wao Bruno atakuwa tayari kwa mchezo huo.

“Sitaki kusema tarehe kamili kwa sababu bado hatujajua, tusubiri tuone,” alisema Amorim alipoulizwa kuhusu tarehe ya kurejea kwa Fernandes.

Tangu ajiunge na Man United akitokea Sporting Lisbon Januari 2020, Fernandes amekuwa nguzo ya muhimu katika kikosi cha kwanza cha Man United.

Kiungo huyo, 31, amekosa mechi tisa pekee kati ya 221 za ligi ambazo Man United imecheza tangu mwaka 2020.

Amorim tayari anakosa huduma za Bryan Mbeumo, Noussair Mazraoui na Amad Diallo wote wakiwa kwenye majukumu ya mataifa yao katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Kukosekana kwa Fernandes ni pigo jingine na kocha Amorim atalazimika kutafuta mbinu mbadala kufidia pengo la mchezaji huyo  aliyefunga mabao matano na kutoa asisti saba za mabao msimu huu.

Baada ya kuikaribisha Newcastle katika Boxing Day, leo, itacheza tena nyumbani siku nne baadaye dhidi ya Wolves, kisha itacheza dhidi ya Leeds na Burnley pamona na moja wa FA Cup dhidi ya Brighton kabla ya kurudi tena katika ligi kucheza dhidi ya Man City.

Akiwazungumzia Harry Maguire na Matthijs de Ligt, ambao walikosa mchezo wa Jumapili kutokana na majeraha, Amorim aliongeza:”Bado tunafanya nao kazi. Hawatocheza mechi hii (dhidi ya Newcastle), lakini tusubiri tuone mechi ijayo.”