Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guimaraes aaga Newcastle, Arsenal yatajwa

GUIMEREZ Pict

Muktasari:

  • Guimaraes, aliyesajiliwa kutoka Lyon mwaka 2022 na kuwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi wa Newcastle, ameibuka kuwa chaguo kuu la kocha Mikel Arteta anayetaka kuongeza nguvu eneo la kiungo kuelekea msimu mpya.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imeongeza kasi katika harakati za kumwania kiungo nyota wa Brazil, Bruno Guimaraes baada ya taarifa kueleza kuwa mchezaji huyo ameomba kuondoka Newcastle United katika dirisha hili la usajili.

Guimaraes, aliyesajiliwa kutoka Lyon mwaka 2022 na kuwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi wa Newcastle, ameibuka kuwa chaguo kuu la kocha Mikel Arteta anayetaka kuongeza nguvu eneo la kiungo kuelekea msimu mpya.

Awali Arsenal ilikuwa ikitafakari uwezekano wa kumsajili Guimaraes au Sandro Tonali, lakini Tonali tayari ametua Tottenham kwa ada ya awali ya pauni 92.5milioni, hali iliyomfanya Guimaraes kuwa lengo kuu la sasa.

GUIME 01

Inaelezwa kuwa wakati wa mazungumzo ya awali na wawakilishi wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, ada ya takribani pauni 60milioni ilitajwa kama kiwango kinachoweza kufanikisha dili hilo.

Licha ya Newcastle kutopokea ofa rasmi kutoka Arsenal hadi sasa, taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo ya London Kaskazini inajiandaa kuwasilisha ofa mpya katika siku zijazo.

Guimaraes kwa sasa anatoka kwenye kipindi kigumu baada ya kukosa penalti katika mchezo ambao Brazil iliondolewa na Norway kwenye hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia.

GUIME 02

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Arsenal inahitaji kuongeza kiungo mmoja tu wa kati, huku pia ikiwafuatilia Alex Scott wa Bournemouth na Ayyoub Bouaddi wa Lille kama mbadala.

Hata hivyo, Newcastle haitakuwa tayari kumuachia kirahisi Guimaraes ambaye ni nahodha wa timu na mmoja wa wachezaji wenye ushawishi mkubwa ndani ya kikosi hicho, hasa baada ya kuwapoteza Sandro Tonali na Anthony Gordon katika dirisha hili la usajili.

GUIME 03

Guimaraes anatarajiwa kutimiza miaka 29 mwezi Novemba, jambo ambalo linaweza kuwa miongoni mwa vigezo vitakavyoamua kiasi ambacho Arsenal itakuwa tayari kulipa ili kukamilisha usajili huo.

Iwapo Arsenal itafanikiwa kupata kiungo mpya, kuna uwezekano wa kumuachia mmoja wa viungo waliopo kikosini, huku Christian Norgaard akitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao klabu ipo tayari kusikiliza ofa zao.

GUIME 04

Aidha, ujio wa kiungo mwingine unaweza kuongeza ushindani katika safu ya kati na kuweka mashakani nafasi ya Martin Zubimendi kuendelea kuwa chaguo la kwanza la Arteta msimu ujao.