Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BREKI: Mourinho sasa kumbakisha Juan Mata, Fellaini Man Utd

JUAN MATA: Kuzaliwa:    Aprili 28,  1988  
Mahali:     Burgos, Hispania
Urefu:     Futi 5, inchi 7  
Nafasi:     Kiungo
Klabu:     Manchester United
Jezi:     Namba  8
Taifa:     Hispania

Muktasari:

  • Inaamnika pia kuwa Mourinho anaamini bado  ana uwezo wa kuupata ubora wa Mata tena, huku pia ikidaiwa kuwa kukosekana kwa klabu kubwa zinazomuhjitaji huenda ikawa sababu ya Mourinho kulazimika kuendelea kuwa naye.

KAMA ulidhani wataondoka basi umechemka. Jamaa wapo wapo sana Manchester United. Ndiyo, Juan Mata, Marouane Fellaini na Daley Blind watakipiga katika jezi ya Manchester United chini ya utawala wa Jose Mourinho.

Kocha huyo Mreno mtata inadaiwa anataka kuwapa nafasi wachezaji hao katika mazoezi ya United ili wamfurahishe, tofauti na mtazamo wa wengi kwamba Mourinho alikuwa mbioni kuwaonyesha mlango ulioandikwa ‘Exit’ pale Old Trafford.

Mourinho ndiye aliyeidhinisha mauzo ya Mata Januari 2014 kwenda Old Trafford licha ya staa huyo kuwa mchezaji bora wa Chelsea kwa misimu miwili mfululizo, lakini inadaiwa kuwa kwanza uhamisho huo ulitokana na donge hilo la United kuwa kubwa huku kiungo Oscar akifanya vema.

Ingawa Mata hajabadilika kitu tofauti na mawazo mengine ya Mourinho kuwa kiungo huyo sio mzuri katika kukaba, lakini habari za ndani kutoka uwanja wa mazoezi wa United, Carrington zinadai kuwa staa huyo atabakia Old Trafford.

Habari hizo zinatazamiwa kumfurahisha Mata, ambaye ameonekana kutulia vema katika Jiji la Manchester na Mei, mwaka huu alikuwepo katika ufunguzi wa Mgahawa wa Tapas jijini Manchester ambao yeye na Baba yake wana hisa.

Inaamnika pia kuwa Mourinho anaamini bado  ana uwezo wa kuupata ubora wa Mata tena, huku pia ikidaiwa kuwa kukosekana kwa klabu kubwa zinazomuhjitaji huenda ikawa sababu ya Mourinho kulazimika kuendelea kuwa naye.

Klabu kubwa, zikiwemo mbili za Hispania, Barcelona na Real Madrid zote zina wachezaji imara namba 10 na kuna uwezekano Mata akabakia kuwa sehemu ya timu huku akitumika katika vikosi vinavyobadilika mara kwa mara.

Kwa upande wa Fellaini, ambaye sio kipenzi cha mashabiki wa Old Trafford tangu alipoletwa kwa dau la pauni 27 milioni na kocha aliyechemsha klabuni hapo, David Moyes, kuna uwezekano mkubwa wa mashabiki wasiompenda wakaambulia maudhi tu.

Inaaminika kuwa Mourinho ni shabiki mkubwa wa soka la nguvu na vurugu la kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, ambaye amekuwa akishutumiwa na mashabiki, makocha na wachezaji wa timu pinzani kwa kutembeza ubabe uwanjani.

Inaeleweka kuwa Mourinho anainyatia saini ya kiungo wake mkabaji wa zamani wa Chelsea, Nemanja Matic, lakini haoni uwezekano wa kocha mpya wa Stamford Bridge, Antonio Conte kumruhusu staa huyo kuondoka, licha ya kukaribia kumnasa kiungo mahiri mkabaji wa Leicester City, N’Golo Kante.

Wakati huo huo, Blind ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi tofauti anatazamiwa kupewa nafasi ya kumuonyesha Mourinho ni kwanini Louis vgan Gaal alilipa pauni 16 milioni kumnunua kutoka Uholanzi katika dirisha la majira ya joto mwaka 2014.

Mourinho anatazamiwa kumtumia Blind katika nafasi tofauti ingawa mchezaji huyo alitumia muda mwingi kucheza kama beki wa kati msimu uliopita, lakini pia anaweza kucheza pembeni pamoja na eneo la kiungo wa ulinzi.

Hata hivyo, habari ya kubaki kwa Mata inatazamia kutoa mvuto mkubwa kwa wachambuzi wa soka huku ukiashiria kasi iliyopo katika maamuzi ya soka kwa sasa.

Habari hii inalinganishwa na habari iliyotokea hivi karibuni kuwa kocha wa Manchester City, Pep Guardila anatazamiwa kubaki na kiungo, Yaya Toure ambaye alimuuza kwenda Manchester City mwaka 2010 wakati akiwa kocha wa Barcelona na ilitazamiwa kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast angekuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa mlango wa kutokea Etihad, lakini mambo yamekuwa tofauti na matarajio ya wengi.