Borussia Dortmund yamng’ang’ania Aubameyang

Muktasari:

Raia huyo wa Gabon amekuwa aihusishwa kuondoka klabuni hapo kwenye dirisha la msimu huu la usajili, ambapo baadhi ya klabu zimeshajitangaza kukaribia kuidaka saini yake.

Ujerumani. Mipango ya Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang kuondoaka klabuni hapo inaelekea kukwama na imeelezwa kuwa ataendelea kuwapo klabuni hapo kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Ujerumani leo Jumanne.

Raia huyo wa Gabon amekuwa aihusishwa kuondoka klabuni hapo kwenye dirisha la msimu huu la usajili, ambapo baadhi ya klabu zimeshajitangaza kukaribia kuidaka saini yake.

Hivi karibuni Mkurugenzi wa klabu hiyo, Hans-Joachim Watzke alisema hakuna maombi rasmi yaliyopelekwa mezani kwake kuhusu uhamisho wa Aubameyang licha ya kusikia taarifa za kuhama kwake.

Taarifa zilizopo hadi sasa, mchezaji huyo mwenye miaka 28 ataendelea kuihudumua BVR.