Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Betis yaanza mkakati kumbakiza Antony La Liga

Muktasari:

  • Antony ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na timu nyingi Ulaya, lakini Betis inataka kupambana kuhakikisha anabaki licha ya ushindani kutoka kwa timu nyingi zinazomtaka.

WAWAKILISHI wa Real Betis watakutana na wale wa Manchester United wiki ijayo kujadili mustakabali wa winga wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 26, Antony, ambaye ameonyesha kiwango bora akiwa katika kikosi chao kwa mkopo msimu huu.

Antony ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na timu nyingi Ulaya, lakini Betis inataka kupambana kuhakikisha anabaki licha ya ushindani kutoka kwa timu nyingi zinazomtaka.

Mkataba wa Antony unatarajiwa kumalizika 2027 na Man United haionekani kuwa na mpango wa kumrudisha katika kikosi licha ya kiwango bora alichoonyesha alipokuwa Betis.

Mbali ya Betis ambayo inapewa nafasi kubwa ya kumsajili kwa mkataba wa kudumu, timu kadhaa za Hispania ikiwemo Atletico Madrid na Valencia zinaitaka huduma ya mshambuliaji huyo. Kwa ujumla katika msimu uliopita mshambuliaji huyo alicheza mechi 40 za michuano yote, akifunga mabao 10  na kutoa asisti tano.


Alejandro Garnacho

WINGA wa Manchester United na timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Garnacho, mwenye umri wa miaka 20, anadaiwa kupokea ofa kutoka Napoli ambayo imewekeza nguvu ili kuhakikisha inaipata saini yake katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Inaelezwa kwamba Garnacho ambaye pia anawindwa na Atletico Madrid, haoni nafasi yake katika kikosi cha Man United chini ya Ruben Amorim.


Emiliano Martinez

KIPA wa Aston Villa na timu ya taifa ya Argentina, Emiliano Martinez, 32, ambaye hivi karibuni aliripotiwa kuwa ataachana na timu hiyo anadaiwa kuwa katika mipango ya Manchester United inayomtaka akampe changamoto Andre Onana golini. Hivi karibuni Emiliano alionekana akiwaaga mashabiki wa Villa jambo lililoibua tetesi kwamba huenda akaondoka msimu huu.


Harvey Elliott

WOLVES wanapambana kuhakikisha inaipata huduma ya kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya England, Harvey Elliott, mwenye umri wa miaka 22. Elliot anataka kuondoka Anfield kwa sababu hapati nafasi ya kutosha kucheza katika kikosi cha kwanza cha Liverpool. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2027.


Jakub Kiwior

BEKI wa Arsenal na timu ya taifa ya Poland, Jakub Kiwior,25, anawindwa tena na Napoli kwa ajili ya dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Licha ya kuhitaji saini yake tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi, Napoli inaitaka Arsenal ikubali kupunguza bei ya mchezaji huyo. Kwa sasa Arsenal inahitaji Pauni 30 milioni ili kumuuza.


Kobbie Mainoo

MANCHESTER United ipo tayari kupokea ofa kwa ajili ya kumuuza mchezaji wake raia wa England, Kobbie Mainoo, 20, hata kama kiungo mwenzake mchezaji wa kimataifa wa Ureno, Bruno Fernandes, 30, ataondoka katika kikosi mara tu dirisha la usajili litakapofunguliwa. Vigogo wa Man United wamekuwa wakitaka kumuuza Mainoo kwa sababu amegoma kusaini mkataba mpya kutokana na ofa ndogo aliyowekewa mezani, huku mkataba wake ukitarajiwa kumalizika 2027.


Christopher Nkunku

MSHAMBULIAJI wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa, Christopher Nkunku ataondoka Chelsea katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi, ambapo timu kibao zimeonyesha nia ya kumsajili ikiwemo Tottenham Hotspur ambayo imeshaanza kuwasiliana na wawakilishi wake. Nkuku ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2029, msimu uliomalizika alicheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao 14.


Theo Hernandez

AL-Hilal iko kwenye mazungumzo na AC Milan ili kuipata saini ya  beki wa kushoto wa timu hiyo na Ufaransa, Theo Hernandez, 27, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Timu hiyo pia inadaiwa kuwa na mazungumzo na kocha wa Inter Milan, Simeone Inzaghi anayetarajiwa kujiunga nayo muda wowote kuanzia sasa ikipambana kujisuka upya.