Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beckham awafunika Ronaldo na Messi

BECKHAM Pict

Muktasari:

  • Utajiri wa familia ya Beckham unaifanya kushika nafasi ya pili kwa wanamichezo tajiri wa Uingereza mwaka huu na nafasi hiyo hiyo pia duniani wakizidiwa tu na Bernie Ecclestone miongoni mwa watu tajiri zaidi katika sekta ya michezo.

LONDON, ENGLAND: WANAPOTAJWA mastaa wa soka wenye utajiri zaidi duniani kwa sasa kuna majina ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ambao mkwanja walionao unazidi Pauni 500 milioni, lakini sasa mwanasoka wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na PSG, David Beckham amewafunika.

Messi ana utajiri wa Pauni 654 milioni huku Ronaldo akiwa na Ukwasi wa Pauni 1 bilioni.

Hata hivyo, utajiri wa Beckham unaotajwa kufikia Pauni 1.185 bilioni unajumuisha ukwasi alionao yeye na mkewe, Victoria, ambaye ni mwanamuziki wa zamani wa kundi la Spice Girls la Uingereza ambaye pia amekuwa akijihusisha shughuli za ubunifu wa mavazi na mitindo.

Utajiri wa familia ya Beckham unaifanya kushika nafasi ya pili kwa wanamichezo tajiri wa Uingereza mwaka huu na nafasi hiyo hiyo pia duniani wakizidiwa tu na Bernie Ecclestone miongoni mwa watu tajiri zaidi katika sekta ya michezo.

BECK 01

Orodha mpya ya matajiri iliyotolewa na Sunday Times inaonyesha kuwa utajiri wao wa Pauni 1.185 bilioni ni karibu nusu ya utajiri wa pauni bilioni 2 bilioni wa mwanzilishi huyo wa Formula One Group, lakini bado unawazidi kwa mbali Barry Hearn na Eddie Hearn.

Beckham alikusanya mamilioni ya pauni ndani na nje ya uwanja katika kipindi chake cha miaka 20 ya kucheza soka, kutokana na ushirikiano na kampuni za Adidas na H&M.

Mikataba hiyo ya kibiashara inaendelea kuwaingizia mapato miaka mingi baadaye baada ya kutundika daruga na soka bado lina mchango mkubwa katika biashara zinazomilikiwa na mkongwe huyo, huku akiwa pia ni mmiliki mwenza wa klabu mbili, Inter Miami na Salford City.

Kuweka kipengele katika mkataba wake wa LA Galaxy kilichomruhusu kununua timu ya upanuzi wa Ligi Kuu Marekani (MLS) kwa Pauni 18.5 milioni kuligeuka kuwa uwekezaji wenye faida kubwa, na miaka minane baada ya kuanzishwa inakadiriwa kuwa na thamani ya Pauni 900 milioni.

BECK 02

Kipindi hicho hicho alinunua hisa ya asilimia 10 katika timu ya Salford ambayo aichezea Hadji Mnoga na msimu uliopita aliongoza ununuzi wa klabu hiyo ya League Two pamoja na Gary Neville, wakinunua hisa zilizobaki za kundi la Class of ’92 la Manchester United.

Hata hivyo, siyo soka pekee lililowaingizia fedha nyingi kwani kampuni ya utayarishaji filamu ya maisha yake ilifanikiwa sokoni kupitia Netflix kuuza mamilioni ya kazi zake. Pia alitengeneza mfululizo wa filamu fupi fupi na mkewe Victoria.

Victoria, ambaye zamani alikuwa mwimbaji alipata utajiri wake wa kwanza akiwa Spice Girls kabla ya kuwa mbunifu wa mitindo, ambapo sasa anamiliki chapa yake binafsi ya mavazi ambayo hivi karibuni imeanza kupata faida baada ya miaka mingi ya kuwa na madeni na hasara.

Victoria pia ana kampuni ya bidhaa za urembo ambayo mwanzoni ilijikita kwenye vipodozi vya macho kabla ya kuzindua bidhaa za kupaka midomo ambazo zinauzwa katika maduka makubwa nchini Ufaransa na Uingereza. Familia ya Beckham siyo pekee kutoka ulimwengu wa soka kuingia katika orodha mpya ya matajiri. Harry Kane ameingia katika 10 bora akiwa na utajiri wa Pauni 110 milioni sawa na Andy Murray.

BECK 03

Nyuma ya familia ya Hearn katika nafasi ya nne yupo mwanzilishi mwenza wa Gymshark Ben Francis akiwa na Pauni 800 milioni mbele ya waanzilishi wenza wa Castore Tom Beahon na Phil Beahon waliopo nafasi ya sita kwa Pauni 350 milioni. Lewis Hamilton ni dereva mwingine wa Formula One aliyeingia kwenye orodha hiyo akiwa na utajiri wa Pauni 435 milioni, huku Rory McIlroy akiwa wa saba Pauni 325 milioni, akichochewa na ushindi wake wa mataji ya Masters mfululizo. Anthony Joshua amemzidi mpinzani wake katika ngumi, Tyson Fury, katika nafasi ya nane, huku utajiri wake wa Pauni 240 milioni ukiwa juu ya Pauni 162 milioni za Fury.


WANAMICHEZO TAJIRI

ENGLAND 2025/2026

1. Bernie Ecclestone na familia          (Pauni 2 bil)

2. David & Victoria Beckham  (Pauni 1.185 bil)

3. Barry & Eddie Hearn          (Pauni 1.035 bil)

4. Ben Francis                        (Pauni 800 mil)

5. Lewis Hamilton                   (Pauni 435 mil)

6. Tom & Phil Beahon (Pauni 350 mil)

7. Rory McIlroy                        (Pauni 325 mil)

8. Anthony Joshua                  (Pauni 240 mil)

9. Tyson Fury              (Pauni 162 mil)

10. Harry Kane                        (Pauni 110 mil)

10. Andy Murray                      (Pauni 110 mil)