Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca hatarini kuadhibiwa na UEFA

Muktasari:

  • Suala hilo limeibuka baada ya timu hiyo kushindwa katika rufaa kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Cas) kuhusu faini ya Pauni 420,000 iliyotolewa na Uefa kwa kuripoti faida kimakosa Oktoba, mwaka jana.

BARCELONA, HISPANIA: BARCELONA inakabiliwa na hatari ya kuadhibiwa na Shirikisho la Kandanda Ulaya (Uefa) baada ya kukiuka sheria za kifedha mwaka wa pili mfululizo.

Suala hilo limeibuka baada ya timu hiyo kushindwa katika rufaa kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Cas) kuhusu faini ya Pauni 420,000 iliyotolewa na Uefa kwa kuripoti faida kimakosa Oktoba, mwaka jana.

Uamuzi wa Cas wakati huo ulionya kuwa timu hiyo ingepata adhabu kali zaidi endapo ingekiuka tena sheria hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Times, Barcelona imepatikana na makosa tena chini ya sheria za Uefa na sasa mabingwa hao wa La Liga wanatarajiwa kupewa adhabu kali.

Adhabu hiyo inaweza kujumuisha kupunguzwa kwa idadi ya wachezaji watakaosajiliwa kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao au hata kupunguziwa pointi katika LaLiga.

Timu za England kama Chelsea na Aston Villa pia zinadaiwa kukiuka sheria hiyo na zinaweza kupata adhabu.

Hata hivyo, kwa kuwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo zitapewa adhabu ya faini ya fedha na sasa mazungumzo yanaendelea huenda hukumu ikatoka mwishoni mwa mwezi huu. Barcelona imekuwa ikijaribu njia mbalimbali kwa ajili ya kujinasua kutoka kwenye matatizo ya kifedha yanayoikabili.

Mwaka 2022 iliuza asilimia 10 ya mapato ya matangazo ya televisheni kwa miaka 25 ijayo kwa Pauni 225 milioni.

Timu hiyo ilitaka mapato hayo yawe kama “mapato mengine ya uendeshaji” kwenye vitabu vya hesabu, jambo ambalo lingeongeza alama kwenye ukokotoaji wa sheria za usawa wa matumizi ya kifedha (FFP).

Hata hivyo, Uefa ilisisitiza kuwa lazima yachukuliwe kama faida kutokana na uuzaji wa mali zisizoonekana ambazo hazihesabiwi katika mfumo wa sheria za usawa wa matumizi ya kifedha.

Barcelona iliuza tena asilimia 15 ya haki za matangazo kwa Pauni 337 milioni, lakini mamlaka za soka zikaieleza kuwa kufanya hivyo hakuisaidii kwani hesabu za mauzo hayo hayatambuliki kwenye sheria kama mapato.

Lakini, uamuzi wa Cas unamaanisha kuwa mapato hayo hayawezi kuhesabiwa kama ya uendeshaji, jambo linalosemekana kuwa chanzo kikuu cha ukiukaji wa hivi karibuni.

Barcelona ilifika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka huu, ikipoteza dhidi ya Inter Milan iliyomaliza kama mshindi wa pili wa mashindano hayo.