ATM YA WIKI: Suarez anastaafu Uruguay na maokoto

Muktasari:
- Suarez mwenye umri wa miaka 37 mbali ya kustaafu timu ya taifa pia haonekani kuwa mbali sana kustaafu upande wa klabu pia kutokana na umri wake.
FLORIDA, MAREKANI: WIKI iliyopita moja kati ya stori kubwa ilikuwa ni Luis Suarez kustaafu timu ya taifa ya Uruguay aliyoanza kuichezea tangu mwaka 2007.
Suarez mwenye umri wa miaka 37 mbali ya kustaafu timu ya taifa pia haonekani kuwa mbali sana kustaafu upande wa klabu pia kutokana na umri wake.
Lakinu hata kama akistaafu staa huyu ana utajiri wa kutosha utakaomfanya aendelee kuishi kishua bila ya shida yoyote.
Leo tumekusogezea hapa jinsi anavyopata pesa na utajiri alionao hadi sasa.

ANAPIGAJE PESA
Kwa sasa staa huyu anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 70 milioni ambayo ni mjumuisho wa madili yake ya nje ya uwanja na mishahara aliyokusanya kuanzia mwanzo wa maisha yake ya soka hadi ssa.
Kwa sasa staa huyu anapokea mshahara unaofikia Dola 1 milioni kwa mwaka hiyo ikiwa ni mjumuosho wa bonasi mbalimbali.
Alikubali kuchukua kiasi hicho na kuacha karibia Dola 200,000 kwa mwezi aliyokuwa anaipata Gremio ili aungane na rafiki yake Lionel Messi.
Mbali ya mshahara wake Suarez amekunja pesa kupitia makampuni mbalimbali kama Puma ambayo kabla ya hapo alikuwa akivalishwa na Adidas.
Mbali ya makampuni hayo Suarez pia ni balozi wa Beats, Beats Abitab, Antel, Cablevision, Garnier, Pepsi, na Samsung ambazo zote kwa pamoja zinampa zaidi ya Pauni 3 milioni kwa mwaka.
MSAADA KWA JAMII
Amewahi kununua zaidi ya vifungashio 1000 vya chakula kwa ajili ya kusaidia watoto wasiojiweza huko Uruguay na mbali ya hiyo amekuwa akicheza mechi mbalimbali za kirafiki zenye lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya kusaidia watu mbalimbali wasiojiweza.

MJENGO
Wakati anajiunga na Inter Miami alinunua mjengo unaokadiriwa kufikia Dola 11 milioni huko Florida Marekani lakini mbali ya mjengo huo anamiliki nyumba nyingine huko Hispania maeneo ya Castelldefels, Catalonia, ambayo aliinunua kwa Dola 3.6 milioni mwaka 2018.

NDINGA
Range Rover Sport-Pauni 67,000
Audi SQ7- Pauni 87,000
BMW X5, Pauni- 70,000
Audi RS6 Avant-Pauni 115,000
Cadillac Escalade-Pauni 90,000
Hyundai Tucson N-Line-Pauni -32,000
BMW iX, Pauni-69,000
MAISHA NA BATA
Yupo kwenye ndoa na Sofía Balbi ambaye ni mchumba wake wa utotoni, wawili hawa walioana mwaka 2009 na hadi sasa wamefanikiwa kupata watoto watatu na wapili ni Benjamin Suarez ambaye anaonekana kufuata nyayo za baba yake na kwa sasa anacheza timu za vijana za Inter Miami ambapo yupo pamoja na mtoto wa Messi. Mtoto wake mkubwa zaidi ni wakike.