Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Atletico yakubali kumuuza Julian Alvarez England

Muktasari:

  • Hata hivyo, licha ya kuwa tayari kumuuza, vigogo wa Atletico wamesisitiza kwamba hawatakubali kupokea ofa yoyote kutoka Barcelona.

ATLETICO Madrid ipo tayari kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Julian Alvarez mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwenda timu yoyote ya Ligi Kuu England ambayo itakuwa tayari kulipa Pauni 85 milioni.

Hata hivyo, licha ya kuwa tayari kumuuza, vigogo wa Atletico wamesisitiza kwamba hawatakubali kupokea ofa yoyote kutoka Barcelona.

Msimamo wa kutotaka kumuuza Barca unatokana na ushindani wa asili ambao timu hizo zimekuwa nao.

Mara kadhaa Arsenal imetajwa kutaka kumsajili, lakini changamoto ni ada yake ya uhamisho.

Arsenal inaamini Alvarez akitua katika kikosi cha ataongeza makali kwani licha ya kufanya vizuri kwa msimu huu, safu yake ya ushambuliaji bado inahitaji kuboreshwa.

Alvarez ambaye ana uzoefu wa kutosha na Ligi Kuu England ameripotiwa kutamani kurudi kwa muda mrefu sasa.


Erling Haaland

BARCELONA imefanya mazungumzo na Manchester City kuhusu straika Erling Haaland na kuwasisitiza kwamba wangependa sana kuwa timu ya kwanza kupewa taarifa ikiwa itafikia mahali watakapofikiria kumuuza straika huyo. Barcelona inamnyatia Haaland kwa msimu wa pili sasa, kakini mara zote Man City imekuwa ikiwaambia kwamba staa huyo hauzwi hata iweje kwa sababu ni moyo wa timu yao. Mkataba wake unaisha 2030.


Mateus Fernandes

MANCHESTER United imekuwa ikimfuatilia kwa muda mrefu kiungo wa West Ham United mwenye umri wa miaka, 21, Mateus Fernandes, ambaye inafikiria kumsajili katika dirisha  lijalo la majira ya kiangazi. Mateus ni mmoja kati ya mastaa wa West Ham United wanaofikiria kuondoka mwisho wa msimu ikiwa timu hiyo itashuka daraja baada ya kuanza vibaya msimu na sasa ikiwa katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa michuano hiyo.


Lamine Camara

NEWCASTLE United imeungana na baadhi ya vigogo Ulaya kumfukuzia kiungo wa AS Monaco, Lamine Camara, 22. Taarifa zinaeleza wababe hao wamekuwa katika mazungumzo na wawakilishi wa Camara kwa miezi kadhaa, lakini bado hakuna mwafaka uliofikiwa huku ikidaiwa PSG ndio ina nafasi kubwa ya kumpata na tayari imeshapiga hatua kadhaa mbele kwenye kuwania saini yake.


Kieran Trippier

BEKI wa Newcastle United, Kieran Trippier, 35, bado hajapokea ofa yoyote ya mkataba mpya kutoka kwa mabosi hali inayoonyesha kwamba hawana mpango wa kuendelea naye. Trippier ambaye anahitajika sana na vigogo wa Scottland, Celtic, amegoma kusaini au kufikia makubaliano na timu nyingine hadi pale atakapojua hatma yake ndani ya Newcastle kwani moyo wake bado unahitaji kuendelea kuichezea timu hiyo.


Alessandro Bastoni

INTER Milan ipo tayari kumruhusu beki kisiki Alessandro Bastoni mwenye umri wa miaka 26, na kiungo, Nicolo Barella, 29, kuondoka katika dirisha kijalo la majira ya kiangazi ikiwa itapata ofa nono. Mastaa hawa wawili wamekuwa wakiwindwa tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana lakini Inter iligoma kuwauza. Timu kadhaa kutoka England ikiwa ni pamoja na Manchester City zimeonyesha nia ya kumsajili Bastoni.


Florian Wirtz

VYANZO vya ndani kutoka Liverpool vimefichua kwamba kiungo mshambuliaji wa timu hiyo ambaye alisajiliwa kwa takribani Euro 100 milioni kutoka Bayer Leverkusen msimu uliopita, Mjerumani Florian Wirtz, 22, huenda akauzwa kwenda Real Madrid katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya miamba hiyo kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. Wirtz hajaonyesha kiwango kilichotarajiwa Liver.


Robert Lewandowski

JUVENTUS ni miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kumsajili straika wa kimataifa wa Poland, Robert Lewandowski, 37,  ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu. Hadi sasa Barca bado haijaanza mazungumzo ya kumsainisha mkataba mpya jambo linaloonyesha kwamba kuna asilimia nyingi anaweza akaondoka. Lewandowski mwenyewe anatamani kusalia Barcelona.