Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Atletico Madrid yaweka msuli mzito kwa Marc Guehi

Muktasari:

  • Guehi amekuwa mmoja wa mabeki wanaowindwa na klabu kadhaa za Ulaya ikiwemo Liverpool, Arsenal na Tottenham tangu dirisha lililopita.

ATLETICO Madrid imeingia kwa nguvu kwenye vita ya kuwania saini ya beki wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Marc Guehi, 25, kuelekea dirisha la usajili la Januari.

Guehi amekuwa mmoja wa mabeki wanaowindwa na klabu kadhaa za Ulaya ikiwemo Liverpool, Arsenal na Tottenham tangu dirisha lililopita.

Hata hivyo, Atletico inatajwa kuja kivingine na ipo tayari kulipa takriban Pauni 50 milioni ili kumsajili staa huyo ifikapo Januari mwakani jambo ambalo litakuwa gumu kwa Palace kukataa kwani ikifanya hivyo mchezaji huyu ataondoka bure ifikapo mwisho wa msimu huu.

Liverpool pamoja na timu nyingine zinazomhitaji staa huyo zinaonekana kutaka kusubiri hadi mwisho wa msimu kisha zimsajili akiwa huru jambo ambalo litakuwa hasara kwa Palace. Mpango wa Atletico inayotaka kutoa mkwanja wa maana unaweza kuwa msaada mkubwa kwa Palace ambayo hadi sasa haina uhakika ikiwa itapata hata Pauni 30 milioni kutoka timu zinazomhitaji Guehi. Hata hivyo swali kubwa linabaki kwa Guehi mwenyewe ikiwa atakuwa tayari kutua Atletico Madrid.


Elliot Anderson

MMANCHESTER City inapanga kumfanya kiungo wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya England, Elliot Anderson, 23, kuwa miongoni mwa mastaa inaotaka kuwasajili dirisha la usajili la majira ya kiangazi. Taarifa zinaeleza benchi la ufundi la Man City linamuhusudu Anderson kuliko Adam Wharton wa Crystal Palace. Hata hivyo, Nottingham Forest inataka takriban Pauni 70 milioni ili kumuuza nyota huyo ambaye mkataba wake unamalizika 2027.


Matteo Guendouzi

SUNDERLAND imepiga hodi Lazio kuonyesha nia ya dhati ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na Ufaransa, Matteo Guendouzi, 26, katika dirisha lijalo. Hata hivyo kuna upinzani mkali kutoka Newcastle United ambayo pia inahitaji huduma yake. Taarifa zinaeleza Sunderland inataka kuongeza nguvu eneo la kiungo katika jitihada za kupambania nafasi za juu ili kufuzu kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao. Lazio inatajwa kuhitaji Pauni 20 milioni ili kumuuza.


Ibrahima Konate

REAL Madrid imeamua kuachana na mpango wa kumsajili beki wa kati wa Liverpool na timu ya taifa ya Ufaransa, Ibrahima Konate, 26, ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa  msimu huu. Inaelezwa Mardid inataka kuwekeza nguvu zaidi kwa Dayot Upamecano. Konate aliyejiunga Liverpool kutoka RB Leipzig 2021 alionekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kuachana na Liverpool dirisha lijalo.


Jean-Philippe Mateta

MSHAMBULIAJI wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ufaransa, Jean-Philippe Mateta, 28, anawindwa na AC Milan na klabu kadhaa za Ligi Kuu England. Palace ipo tayari kumwachia Januari ingawa itahitaji Pauni 30 milioni. Nyota huyo alionyesha kiwango bora msimu uliopita kiasi cha kuivutia Manchester United iliyokuwa karibu kumsajili kabla ya dili kufa katika dakika za mwisho.


Kenan Yildiz

ARSENAL imeanza mazungumzo na wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa Uturuki, Kenan Yildiz, 20, wa Juventus ambaye inataka kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Yildiz ambaye ameonyesha kiwango bora tangu ajiunge na Juventus, mabosi wa Juventus hawaonekani kuwa tayari kwa sasa kumuuza ingawa mwenyewe ameonyesha nia ya kutaka kuondoka. Kwa sasa vigogo wa Juve wanafanya mazungumzo naye.


Kobbie Mainoo

NAPOLI imewasilisha tena maombi kwa Manchester United kuulizia uwezekano wa kuipata huduma ya kiungo  wa timu hiyo na England, Kobbie Mainoo, 20, ambaye kwa sasa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza. Hata hivyo, taarifa kutoka Old Trafford zinaeleza Man United haipo tayari kumuuza mchezaji huyo licha ya mwenyewe kuomba kuondoka.


Tino Livramento

HUKO Newcastle United inaripotiwa mshambuliaji wa pembeni wa England, Tino Livramento, 23, anahitajika Manchester City, huku ikikabiliwa na ushindani kutoka Manchester United na Arsenal. Livramento amekuwa akipata nafasi finyu kikosi cha kwanza cha Newcastle, lakini kasi, uwezo wa kushambulia na kuzuia ni sifa zinazomfanya kuwa chaguo la kuvutia kwa klabu kubwa.