Atalanta yaiduwaza Liverpool nyumbani

Thursday November 26 2020
Uefa pic

LIVERPOOL, ENGLAND. KLABU ya Atalanta ya Italia imeisapraizi Liverpool kwa kuishushia kipigo cha mabao 2-0 ndani ya dakika nne kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuweka hai matumaini yao ya kutinga hatua ya mtoano ya 16 Bora.
Katika mchezo wa kwanza ambao ulichezwa Italia, Atalanta wakiwa nyumbani  walichezea kichapo cha mabao 5-0.
Liverpool ilijikuta ikikumbana na wakati mgumu kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Anfield  na kushindwa kupiga hata  shuti  moja lililolenga lango la Atalanta.
Mabao ya Josip Ilicic na Robin Gosens kipindi cha pili ambayo yalifungwa dakika ya  60 na 64 yalitosha kwa Atalanta inayonolewa na Gian Piero Gasperini kuvuna pointi tatu muhimu wakiwa ugenini.
Katika mchezo huo, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alionekana akifanya mabadiliko kwa  wachezaji wanne  ambao ni Salah, Wijnaldum, Origi na Tsimikas  huku wakiingia Firmino, Fabinho, Jota na Robertson lakini mabadiliko hayo yajakuzaa matunda .

UEFA PI1


Pamoja na kipigo hicho, Liverpool wataendelea kuongoza msimamo wa kundi lao D wakiwa na pointi 9 huku wakifuatiwa na Ajax pamoja na Atalanta wenye pointi saba kila mmoja ili kujihakikishia kutinga hatua ya mtoano wanatakiwa kufanya vizuri katika mchezo wao ujao.
Liverpool itacheza ugenini dhidi ya Ajax kabla ya kukabiliana na   Midtjylland ambao wanaburuza mkia kwenye kundi lao wakiwa hawana pointi hata moja.

MATOKEO KAMILI

B. Monchengladbach 4 - 0 Shakhtar Donetsk
Olympiacos Piraeus  0 - 1 Manchester City
Ajax                     3 - 1 Midtjylland
Atl. Madrid                0 - 0 Lokomotiv Moscow
Bayern Munich          3 - 1 Salzburg
Inter                          0 - 2 Real Madrid
Liverpool                   0 - 2 Atalanta
Marseille                    0 - 2 FC Porto

Advertisement