Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta: Bado tuna kazi kubwa kutwaa ubingwa EPL

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Arsenal ambayo sasa ina alama 73 ikiwa na tofauti ya alama tatu na Manchester City ambayo bado ina kiporo kimoja, hivi karibuni imeonekana kuwa katika hatari ya kulikosa la Ligi Kuu England baada ya kufanya vibaya katika mechi kadhaa.

LONDON, ENGLAND: LICHA ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0, jana dhidi ya Newcastle na kukaa kileleni, Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesisitiza bado wana kazi kubwa ya kufanya ili kushinda taji la Lig Kuu England.

Arsenal ambayo sasa ina alama 73 ikiwa na tofauti ya alama tatu na Manchester City ambayo bado ina kiporo kimoja, hivi karibuni imeonekana kuwa katika hatari ya kulikosa la Ligi Kuu England baada ya kufanya vibaya katika mechi kadhaa.

Akizumgumza baada ya mechi hiyo, Arteta amesema: “Tuko hapa tulipo. Sitarajii mambo yawe rahisi au ya kupendeza kwa sababu tunahitaji kushinda taji baada ya miaka 23. Najua kila siku vitu vitakuwa vigumu hivi hivi na sisi tuko tayari kwa hilo."

ART 01

"Ni vigumu sana kushinda ligi hii. Tulihitaji kufunga bao la pili. Tulijaribu, lakini kama huna ufanisi katika baadhi ya maeneo, lazima uwe na mbinu nyingine za kushinda.”

Aliongeza, timu yake ina nidhamu na ujasiri mkubwa hasa katika kipindi hiki muhimu kwao wakilikaribia taji la EPL.

Arsenal walidaiwa kupata pigo jingine kubwa baada ya mechi hiyo dhidi ya Newcastle kwani staa wao Kai Havertz alipata majeraha yaliyosababisha asimalize mechi.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani aliwahi kuumia vibaya goti mwanzoni mwa msimu na kukaa nje hadi Januari. Tangu arejee, amefunga mabao matano, lakini sasa anaweza kukosa tena mechi kadhaa baada ya kuumia dakika ya 32 ya mechi dhidi ya Newcastle United.

Havertz alionekana akiwa mwenye huzuni alipotolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Viktor Gyokeres. Jambo lililowashtua wengi ni staa huyo kupelekwa katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa ajili ya kufanyiwa matibabu zaidi.

ART 02

Arteta pia amesema kwa sasa timu yake inatakiwa kuwa makini sana katika eneo la mwisho na kutumia kila nafasi watakayopata kwani ushindani wa ubingwa ni mkubwa mno.

Akizungumzia majeraha ya Havertz pamoja na Eberechi Eze ambao wote walishindwa kumaliza mechi dhidi ya Newcastle, Arteta amesema wachezaji hao hawaonekani kuumia sana, hivyo kuna asilimia kubwa wakarejea kikosini na wakacheza mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid, Jumatano ya wiki hii.