Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal v Man City mziki uko hapa

TAJI 02

Muktasari:

  • Mbio za ubingwa huo siyo tu zimepamba moto, lakini zinafikia kilele chake. Hadi wikendi iliyopita, ilionekana kana kwamba Arsenal walikuwa wanafanya mambo kwa ustadi mkubwa, na ubingwa ulikuwa karibu kabisa kuwa wao, lakini ghafla sare dhidi ya Bournemouth ilibadilisha  mwelekeo wa mbio hizo.

LONDON, ENGLAND: It’s Winner’s Day. Ni siku ya bingwa. Ndivyo ilivyo wakati lile pambano la Ligi Kuu England kati ya Arsenal na Manchester City linalopigwa leo kwenye Uwanja wa Etihad linaweza kuibua hoja katika mbio za kuwani ubingwa msimu huu.

Mbio za ubingwa huo siyo tu zimepamba moto, lakini zinafikia kilele chake. Hadi wikendi iliyopita, ilionekana kana kwamba Arsenal walikuwa wanafanya mambo kwa ustadi mkubwa, na ubingwa ulikuwa karibu kabisa kuwa wao, lakini ghafla sare dhidi ya Bournemouth ilibadilisha  mwelekeo wa mbio hizo.

Na sasa Gunners wako katika mpambano mkali na Manchester City ambao watakutana nao kesho katika Uwanja wa Etihad kwenye moja ya mechi kubwa zaidi za kuamua ubingwa katika soka la kisasa.

ARS 01

Kikosi cha Mikel Arteta kinaongoza kwa tofauti ya pointi sita dhidi ya Manchester City ambao wana mchezo mmoja mkononi. Wanajua kuwa kuepuka kufungwa kutawaweka karibu zaidi na kushinda ligi hiyo kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 22, na hiyo ni mechi ya kuamua ubingwa yenye athari kubwa juu ya nani atachukua taji mwishoni mwa Mei.

Hata hivyo, kuna uwezekano ingawa ni mdogo, kwamba hiyo haitakuwa mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana kuwania ubingwa msimu huu. Bado kuna uwezekano wa mechi ya mtoano (play-off) kati ya Arsenal na Manchester City.

ARS 02


Kwa kawaida, ubingwa wa EPL huamuliwa kwa pointi kwanza. Ikiwa timu zitalingana huangaliwa tofauti ya mabao na baadaye vigezo vingine kadhaa hutumika. Njia pekee ya kufanya play-off iwezekane ni ikiwa Manchester City na Arsenal watatoka sare ya bao 1-1 Etihad wikendi hii.

Kwa nini? Kwa sababu matokeo hayo yatafanya rekodi ya kukutana uso kwa uso iwe nzuri kufuatia sare ya 1-1 katika Uwanja wa Emirates, Septemba, ambapo bao la dakika za nyongeza la Gabriel Martinelli lilisawazisha lile la mapema la Erling Haaland.

Iwapo hali hiyo itatokea, na bado timu hizo zikawa sawa hata kwa mabao ya kufunga, basi mechi ya mtoano itachezwa. Mechi hiyo itakuwa  moja katika uwanja huru utakaochaguliwa na kampuni inayoendesha ligi hiyo, Premier League. Hata hivyo, bado iko mbali na kufikia hatua hiyo, kwani Arsenal wanaongoza ligi kwa pointi 70 dhidi ya Manchester City wenye 64.

ARS 03

Ili play-off iwezekane, Arsenal watalazimika pia kupoteza angalau mchezo mmoja kati ya mechi tano zilizobaki baada ya pambano hilo, huku Manchester City wakishinda mchezo uliopo mkononi. Wapinzani wote waliobaki kwa Arsenal kwa sasa wako nusu ya chini ya msimamo.

Arsenal watacheza na Newcastle (nyumbani), Fulham (ugenini), West Ham United (ugenini), Burnley (nyumbani), na kumaliza na Crystal Palace (ugenini). Pia walishawahi kuzifunga timu zote hizo katika mechi za awali.

Kwa upande mwingine, Manchester City waliotwaa ubingwa mara sita chini ya Pep Guardiola wanakabiliwa na ratiba ngumu zaidi wakicheza na Burnley, Everton, Brentford, Bournemouth, Crystal Palace na kumaliza na Aston Villa wanaowania nafasi za kushiriki mashindano ya Ulaya msimu ujao.

ARS 04

Katika vigezo vingine vya kuvunja sare, Arsenal wana faida ndogo ya tofauti ya mabao. Wamefunga bao moja zaidi na kuruhusu mawili ikiwa ni machache zaidi kuliko City. Lakini hali hiyo inaweza kubadilika ikiwa Manchester City wataifunga Arsenal mbele ya mashabiki wake.

Kila kitu sasa kinaelekea kwenye pambano hilo kubwa la Etihad wakati ambao vinara wa ligi wanaonekana kutafuta upya kiwango bora baada ya kushinda mchezo mmoja kati ya mitano iliyopita. Arsenal bado wanaongoza msimamo, lakini wasipoboresha kiwango, Manchester City wana nafasi kubwa ya kuwafunga Jumapili hii kama walivyofanya kwenye fainali ya Kombe la Carabao mwezi uliopita.