Arteta apiga muziki mazoezini
Muktasari:
- Mpango wa Arteta ni kuhakikisha anajaribu kuweka utulivu wa kutosha kwenye timu yake ili kufikia mafanikio yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.
LONDON, ENGLAND: Mpango wa Arteta ni kuhakikisha anajaribu kuweka utulivu wa kutosha kwenye timu yake ili kufikia mafanikio yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.
Mpango wa Arteta ni kuhakikisha anajaribu kuweka utulivu wa kutosha kwenye timu yake ili kufikia mafanikio yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.
Arteta anajaribu kupafanya London Colney kama mahali pa kufurahia baada ya kuamua kuwawekea muziki, wachezaji wafanye mazoezi wakiwa na tabasamu.
Arsenal ilitarajia kukipiga na Dinamo Zagreb kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na katika mchezo huo, Arteta ataweka spika kwenye uwanja wa mazoezi na kuweka ala maarufu za muziki za Kibrazili wakati wakijifua, alipowawekea wimbo wa Mais Que Nada wa msanii Sergio Mendes.
Kwenye hilo, Arteta alisema: “Hiki ni kitu ambacho kimekuwa kikifanyika kwa miaka mingi sasa. Kama sehemu ya mazoezi, tumekuwa tukisikiliza muziki katika baadhi ya mazoezini yetu hasa ya kuboresha nguvu, hivyo tunahitaji kuwafanya wachezaji kufurahia mazoezini.”
Arsenal na Arteta inahitaji kubadili hali ya mambo kwenye kikosi chao ili kishindane kwa mafanikio kwenye michuano iliyobaki baada ya kutupwa nje kwenye Kombe la FA na Manchester United kwa mikwaju ya penalti na ilipoteza pia kwa mabao 2-0 kwenye nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Ligi mbele ya Newcastle United.
Mbio zao kwenye kufukuzia taji la Ligi Kuu England nazo zilikumbana na kigingi kwenye mechi iliyopita, ilipopoteza ushindi wake wa mabao 2-0 na kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Aston Villa, Jumamosi iliyopita na hivyo kujikuta ikiachwa pointi sita nyuma na vinara Liverpool.
Novemba 2021, Arteta alijaribu kuwaandaa wachezaji wake kwa ajili ya mechi ya Anfield, ambapo aliwawekea wimbo wa ‘You’ll Never Walk Alone’ wakati wakifanya mazoezini, lakini ilichokwenda kukutana nacho kwenye mchezo huo ni kipigo cha mabao 4-0 na kwenda hilo la muziki, Arteta alisema: “Muziki ni sehemu ya utamaduni wetu. Tumekuwa na muziki kila mahali na muziki una nguvu kubwa ya kubadili ari, nguvu na kila kitu.”
Winga Leandro Trossard, alisema: “Sifahamu ni nani anayeweka muziki wakati wa mazoezini. Yakupasa tu kuzoea hali hiyo.”