Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta apewa ubingwa, Pep asema tutaona!

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Kikosi cha Pep Guardiola kiliongoza kwa mabao mawili hadi mapumziko ya kipindi cha kwanza dhidi ya Tottenham, baada ya kufunga kupitia kwa Rayan Cherki na Antoine Semenyo. 

LONDON, ENGLAND: JAMIE Redknapp anaamini mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England zimekwisha baada ya Manchester City kuangusha pointi tena katika juhudi zao za kuifukuzia Arsenal chini ya Kocha Mikel Arteta.

Kikosi cha Pep Guardiola kiliongoza kwa mabao mawili hadi mapumziko ya kipindi cha kwanza dhidi ya Tottenham, baada ya kufunga kupitia kwa Rayan Cherki na Antoine Semenyo.

Hata hivyo, Man City iliporomoka kipindi cha pili na Dominic Solanke alifunga mara mbili kuisaidia Spurs kupata sare nyumbani.

Kipindi hicho kibaya cha pili, kikichanganywa na ushindi mkubwa wa Arsenal wa mabao 4-0 dhidi ya Leeds saa 24 zilizotangulia, kimeifanya Man City sasa kuwa nyuma kwa pointi sita katika msimamo wa ligi, pengo ambalo Redknapp anaamini linatosha kabisa kuamua ubingwa.

Akizungumza na Sky Sports, Redknapp amesema: “Mikel Arteta bila shaka alikuwa nyumbani mchana huu akiangalia mechi hizi mbili na kufikiria, ‘Ninaipa Aston Villa nafasi ya kuifunga Brentford’ lakini hawakufanya hivyo. Kisha akaona hiki kipindi cha pili akifikiria, ‘5-0’. Leo usiku atakuwa anafungua chupa nzuri ya mvinyo wa Rioja. Hii ndiyo hiyo. Nafikiri huu ni ubingwa wa Arsenal sasa na ninaona wanaweza kuushinda kwa tofauti ya pointi nane au 10.

"Nitashangaa sana kama hawatafanya hivyo. Wana wachezaji bora. Nafikiri walikuwa wanaanza kuwa na wasiwasi kidogo, mashabiki, uhusiano kati yao na timu. Kocha pia anakuwa na presha kidogo na hilo linaathiri wachezaji. Lakini sasa wanaweza kupumua, na nitashangaa kama hawatashinda ubingwa huu kwa urahisi.”

Ingawa Redknapp alimhimiza Arteta afungue chupa ya mvinyo na kusherehekea mapema, kuna uwezekano mdogo kocha huyo Mhispaniola kufanya hivyo.

Hata Pep Guardiola hakuzungumza kama kocha aliyekata tamaa baada ya mechi, akisema: “Kwa jumla tulicheza vizuri sana. Kuanzia dakika ya 70 walipiga mipira mingi nyuma ya mabeki, wakaongeza wachezaji pale na wakashambulia moja kwa moja zaidi. Walipata bao na tunajua kilichofuata. Baada ya hapo walikuwa na kasi ya mchezo. Ligi Kuu England iko hivyo. Baadaye tulirudisha kasi yetu tena.

"Ni pigo, lakini bado tupo kwenye mbio. Tunasonga mbele. Kuna mechi 14 zilizobaki na pointi nyingi bado zipo. Tutaona.”