Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta akipata hii timu mtaomba po!

Muktasari:

  • Dirisha la usajili wa Januari lipo wazi kwa sasa na Arsenal inatazamiwa kuwa bize kusaka nyota wapya. Kikosi hicho cha kocha Arteta kwa sasa kinapambana kishinde ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kukaribia kufanya hivyo kwa misimu miwili mfululizo.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL inaweza kutumia mamilioni ya pesa kwenye usajili wa dirisha hili la Januari na kumfanya kocha Mikel Arteta kuwa na kikosi kipya kabisa cha kwanza itakapofika mwishoni mwa mwezi huu.

Dirisha la usajili wa Januari lipo wazi kwa sasa na Arsenal inatazamiwa kuwa bize kusaka nyota wapya. Kikosi hicho cha kocha Arteta kwa sasa kinapambana kishinde ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kukaribia kufanya hivyo kwa misimu miwili mfululizo.

Ujio wa nyota wapya kwenye kikosi hicho cha Emirates utaipa Arsenal nguvu ya kuchuana na Liverpool kwenye mbio za ubingwa. Kwa sasa itakosa huduma ya winga wake Bukayo Saka, lakini kama wachezaji wapya wakija, watamfanya Arteta kuwa na wigo mpana wa machaguo ya kikosi chake.

Kuna wachezaji kibao wanahusishwa na Arsenal na huenda ikawa timu mpya mwanzoni mwa Februari. Staa wa Athletic Bilbao, Nico Williams anahusishwa na miamba hiyo ya Emirates na akinaswa hakika atakuja kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Arteta.

Wakati Williams akiwa kwenye wingi moja, wingi nyingine kutakuwa na staa wa Wolves, Matheus Cunha, ambaye pia yupo kwenye rada za kocha Arteta akiamini atanasa huduma yake kwenye dirisha hili la Januari ili kumpa ushindani wa kuwania namba Mbrazili mwenzake Gabriel Martinelli.

Ishu ya moto kuhusu Arsenal kwa sasa ni kama itafanikiwa kunasa saini ya straika Alexander Isak ili kwenda kuongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, huku kasheshe kubwa likidaiwa bei anayouzwa mkali huyo, Pauni 150 milioni inaweza kuwa kikwazo. Lakini, dhamira ya Arsenal ni kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England, hivyo inaweza kufumba macho na kutoa mkwanja huo kwenda kunasa saini ya Isak.

Eneo jingine ambalo Arteta atahitaji huduma mpya ni kwenye eneo la kiungo na sasa anamsaka Martin Zubimendi kuja kuleta uimara kwenye kiungo ya kukaba ili kumfanya Martin Odegaard kuwa bize kwenye kutengeneza nafasi za kufunga.

Kama Arteta atafanikiwa kunasa huduma za mastaa anaowasaka, basi kikosi chake cha kwanza kitakuwa hivi: Raya; Calafiori, Gabriel, Saliba, Timber; Rice, Zubimendi, Odegaard; Williams, Cunha, Isak.