Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsene Wenger aponda usajili wa Wirtz Liverpool

WENGER Pict

Muktasari:

  • Liverpool ililipa Pauni 116 milioni kunasa saini ya kiungo huyo mchezeshaji kutoka Bayer Leverkusen, ambako alikuwa akicheza kwa kiwango cha juu sana.

LIVERPOOL, ENGLAND: NGULI wa soka, Arsene Wenger amesema Liverpool imeamua kuiharibu safu yao ya kiungo bora kabisa kwa uamuzi wao wa kumsajili Florian Wirtz kama Namba 10 mpya msimu huu huku Mjerumani huyo akishindwa kufanya kitu cha maana tangu aliponaswa kwa pesa ndefu.

Liverpool ililipa Pauni 116 milioni kunasa saini ya kiungo huyo mchezeshaji kutoka Bayer Leverkusen, ambako alikuwa akicheza kwa kiwango cha juu sana.

Hicho kilikuwa kiwango cha juu kabisa kwa Liverpool kulipa kusaini mchezaji mmoja na kuvunja rekodi ya uhamisho Uingereza, kabla ya kuvunja tena rekodi yao wenyewe ilipomsajili straika Alexander Isak kwa Pauni 130 milioni.

Licha ya Wirtz kuonekana kuwa moto huko alikotoka, alipotua Liverpool alifanywa kuwa mchezeshaji wao mkuu, eneo ambao bado hajalitendea haki, akiwa hajafunga wala kuasisti katika mechi 10 ilizocheza timu yake kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

WENG 01

Wakati Liverpool ilipokumbana na matokeo mbaya kocha Arne Slot alishutumiwa kikosi chake kutokuwa na uwiano bora licha ya kutumia pesa nyingi kwenye usajili wa dirisha lililopita.

Wirtz alicheza pembeni wakati Liverpool ilipoichapa Real Madrid, Jumanne iliyopita, lakini kocha Wenger amesema miamba hiyo ya Anfield ilifanya makosa kwa kumwambia Mjerumani huyo kwamba atakwenda kuwa Namba 10 wao, kitu ambacho kimeshindwa kuleta matunda.

Wenger amesema: “Liverpool ni mfano mzuri. Wakati Wirtz alipokuwa na machaguo ya kwenda Bayern Munich au Liverpool, aliiambia Liverpool: ‘Nitakuja kama nitacheza Namba 10. Sitaki kucheza pembeni’. Liverpool, ili kumpata, ilisema sawa.

“Walianza kumtumia kwenye safu yao ya kiungo, ambayo awali ilikuwa na (Ryan) Gravenberch, (Alexis) Mac Allister, (Dominik) Szoboszlai. Kwa kumchezesha Wirtz, wakalazimika kumweka nje Szoboszlai. Walichofanya mechi dhidi ya Aston Villa, walirejea kwenye kiungo yao ya msimu uliopita. Na dhidi ya Madrid, ilimtumia Wirtz, lakini alichezeshwa pembeni.

“Kocha amesema: ‘Kama unataka kucheza tena, utapaswa kucheza pembeni kwa sababu sitaki tena kuivuruga safu yangu ya kiungo.’ Hicho ndicho kilichotokea usiku ule wa Madrid. Wirtz amerejea kwenye timu, lakini ametumika pembeni kushoto kama ambavyo alikuwa akitumika Leverkusen.”

WENG 02

Uamuzi huo umeleta matunda baada ya Liverpool kushinda mechi mbili mfululizo dhidi ya Aston Villa na Real Madrid kwa mara ya kwanza tangu mwishoni mwa Septemba.