Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Petit: Wirtz? Hana ile thamani buana

WITZ Pict

Muktasari:

  • Wirtz, 22, amekuwa kwenye presha, licha ya gwiji wa soka la Ujerumani kumtetea kutokana na kukosolewa kwa kiwango chake cha huko England. Ada yake ya uhamisho ambayo iliweka rekodi kabla ya Liverpool kuivunja kwenye usajili wa Alexander Isak kutoka Newcastle United kwa ada ya Pauni 130 milioni.

LIVERPOOL, ENGLAND: USAJILI wa Liverpool wa staa wa Pauni 116 milioni, Florian Wirtz ameanza vibaya maisha yake huko Anfield, hajafunga wala kuasisti kwenye Ligi Kuu England tangu alipojiunga kutoka Bayer Leverkusen.

Kiungo huyo Mjerumani amewekwa benchi kwenye mechi za karibuni dhidi ya Everton na Chelsea.

Wirtz, 22, amekuwa kwenye presha, licha ya gwiji wa soka la Ujerumani kumtetea kutokana na kukosolewa kwa kiwango chake cha huko England. Ada yake ya uhamisho ambayo iliweka rekodi kabla ya Liverpool kuivunja kwenye usajili wa Alexander Isak kutoka Newcastle United kwa ada ya Pauni 130 milioni.

WIT 01
WIT 01

Hata hivyo, staa wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Emmanuel Petit amesema Wirtz hakuwa na thamani ya pesa ambayo Liverpool ililipa kupata saini yake. Petit anaamini kiwango kibovu cha Wirtz huko Anfield ni kitu ambacho kiungo huyo mwenyewe anapaswa kukubali. “Ligi Kuu England ni changamoto tofauti kabisa na Bundesliga,” amesema Petit na kuongeza “Leverkusen ilikuwa ikicheza soka la kushambulia kwa kushtukiza hilo lilimpa nafasi ya kufanya vizuri. Liverpool inataka kumtawala mpinzani, hivyo mbinu ni tofauti.

WIT 01

“Florian Wirtz amekuja kwenye utamaduni na mazingira tofauti kabisa kitu kinachomwongezea presha. Binafsi, sitaki kuamini kama alikuwa na thamani ya ada yake uhamisho, licha ya kwamba namheshimu kama mchezaji. Nadhani wachezaji wanakuwa kwenye presha kutokana na dili zinazoingiwa na klabu. Kama ukimuuliza mwenyewe, atakwambia hana thamani ya pesa ambayo ililipwa kupata saini yake, huo ndio ukweli.

“Nafahamu itamchukua muda mrefu kuifanya staili yake ya uchezaji kufanya kazi kwenye Ligi Kuu England. Ana kipaji hivyo, naamini atafanikiwa, lakini atahitaji kucheza mechi nyingi kuzoeana na wenzake.

“Ligi Kuu England si Bundesliga na Liverpool inacheza tofauti na Leverkusen.” Kocha wa Liverpool, Arne Slot alidai kwamba anaamini Wirtz ni suala la muda tu kabla ya kuanza kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu England.