Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yafunika kulipa wagonjwa

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Emirates ilitumia Pauni 35 milioni msimu uliopita kulipa mishahara wachezaji waliokuwa hawachezi kutokana na kuwa majeruhi, ikiwa ni kiwango kikubwa cha pesa kuliko vilivyolipwa na timu nyingine kwenye Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND: HABARI ndo hiyo. Hatimaye, Arsenal imebeba taji la kuwa timu iliyotumia pesa nyingi zaidi kuwalipa mishahara wachezaji majeruhi.

Miamba hiyo ya Emirates ilitumia Pauni 35 milioni msimu uliopita kulipa mishahara wachezaji waliokuwa hawachezi kutokana na kuwa majeruhi, ikiwa ni kiwango kikubwa cha pesa kuliko vilivyolipwa na timu nyingine kwenye Ligi Kuu England.

Wachezaji waliokuwa majeruhi kwa msimu uliopita ni pamoja na Martin Odegaard, Bukayo Saka, Raheem Sterling, Kai Havertz, Gabriel Jesus, Declan Rice na Oleksandr Zinchenko.

Kwa mujibu wa Transfermarkt iliyotoa uchambuzi wa wachezaji majeruhi kwenye Ligi Kuu England kwa msimu uliopita na kupitia mtandao wa Capology unaofichua mishahara ya mastaa hao, Arsenal ilionekana kutumia pesa nyingi kulipa wagonjwa msimu uliopita.

Manchester City inashika namba mbili kwa kutumia Pauni 33 milioni na kufuatia Manchester United, iliyolipa Pauni 25 milioni kwenye mishahara ya wachezaji wagonjwa.

Tottenham Hotspur ililipa Pauni 18 milioni, Chelsea Pauni 17 milioni, Brighton Pauni 14 milioni na Newcastle United ililipa Pauni 13 milioni.

Mabingwa wa Ligi Kuu England, Liverpool ililipa Pauni 12 milioni kulipa mishahara ya wachezaji majeruhi, Aston Villa ilitumia Pauni 10 milioni na Everton ilikuwa na bili ya Pauni 9 milioni kulipa mishahara ya wachezaji waliokuwa kwenye wodi ya wagonjwa.

Shabiki wa Arsenal, Craig Burke, 43, alisema: “Tumekuwa tukishinda hili taji tangu 2020, na kinachoumiza zaidi, Spurs imebeba kombe — hiyo inauma sana. Mbaya, tumelipa Pauni 35 milioni mishahara ya wachezaji waliokuwa wameketi tu nje ya uwanja na haionekani kama hilo litakwenda kuwa tofauti kwa msimu mpya.”