Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal mpo? Bei ya Sesko imepanda

Muktasari:

  • Sesko, 21, alifunga bao matata kabisa kwenye mchezo wa sare ya 3-3 dhidi ya Bayern Munich jambo linamfanya mchezaji huyo asakwe na timu kibao katika kuelekea dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL italazimika kulipa zaidi kunasa saini ya straika Benjamin Sesko kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya RB Leipzig kuongeza dau katika kipengele kilichopo kwenye mkataba wake.

Sesko, 21, alifunga bao matata kabisa kwenye mchezo wa sare ya 3-3 dhidi ya Bayern Munich jambo linamfanya mchezaji huyo asakwe na timu kibao katika kuelekea dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Fowadi huyo wa kimataifa wa Slovenia alihusishwa sana na Arsenal kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini dili hilo lilishindwa kukamilika.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta na skauti wake wamekuwa wakimfuatilia mshambuliaji huyo, ambaye amefunga mabao 21 katika mechi 45 alizocheza msimu huu.

Lakini, kupata timu nyingine ya kuhamia kwenye dirisha hili, ugumu unakuja kwenye bei iliyotajwa katika mkataba wake, ambapo Leipzig imeipandisha. Klabu hiyo ya Ujerumani inamthaminisha Sesko sasa kwa Pauni 68 milioni, ikipanda kutoka Pauni 60 milioni, bei ambayo alikuwa akiuzwa kwenye dirisha la Januari mwaka huu.

Leipzig inataka pesa hiyo na mtindo tofauti kabisa wa malipo ambao unakwenda kinyume na mipango ya Arsenal. Straika Sesko bado anaendelea kuwamo kwenye orodha ya mastraika watano waliopo katika orodha ya wanaosakwa na miamba hiyo ya Emirates kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Mastraika wengine waliopo katika rada ni mkali wa Newcastle United, Alexander Isak, straika wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres, staa wa Wolves, Matheus Cunha na yule wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike.