Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Manchester United zalainishiwa kwa Gyokeres

Muktasari:

  • Timu kibao zimekuwa zikitajwa kufukuzia ili kumsajilimchezaji huyo ikiwemo Arsenal na Manchester United, hivyo huenda zikapata urahisi.

MABOSI wa Sporting Lisbon wapo tayari kupunguza bei ya mshambuliaji wa timu hiyo na timu ya taifa ya Sweden, Viktor Gyokeres katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kutoka Pauni 85 milioni hadi Pauni 59 milioni ili ondoke kikosini.

Timu kibao zimekuwa zikitajwa kufukuzia ili kumsajilimchezaji huyo ikiwemo Arsenal na Manchester United, hivyo huenda zikapata urahisi.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028.

Staa huyo kwa sasa ana umri wa miaka 27 na inadaiwa amewaambia mabosi wa timu hiyo kwamba anataka kuondoka mwisho wa msimu.

Gyokeres anaamini muda huu ndio sahihi kuondoka na ikiwa atachelewa kusepa huenda timu kubwa zinazomtaka zikajiondoa katika mipango hiyo.

Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 43 za michuano, akifunga mabao 43 na kutoa asisti 11.


WOLVES imeibuka katikati ya timu zinazoitaka saini ya winga wa Manchester United, Jadon Sancho katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Sancho ambaye kwa sasa anaichezea Chelsea kwa mkopo ameanza kutafuta timu nyingine ya kujiunga nayo kwa sababu matajiri hao wa Jiji la London hawana mpango wa kumsainisha mkataba wa kudumu wakati Man United pia hayupo katika mipango yao.


MSHAMBULIAJI wa Manchester United na timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Garnacho, 20, amezidisha uvumi wa kuondoka mwisho wa msimu huu baada ya kuiweka sokoni nyumba yake. Inaelezwa Sancho anayewindwa na Atletico Madrid, amefanya uamuzi wa kuachana na Man United mwisho wa msimu baada ya hivi karibuni kutokuwa na maelewano mazuri na kocha Ruben Amorim.


MSHAMBULIAJI wa Olympique Lyon na timu ya taifa ya Ufaransa, Rayan Cherki, 21, ambaye anawindwa na Tottenham na Manchester United ana kipengele katika mkataba  kinachomwezesha kuondoka ikiwa timu inayomtakai italipa Pauni 25 milioni. Cherki ni mmoja kati ya washambuliaji waliofanya vizuri msimu huu ambapo amefunga mabao manane.


KIPA wa Espanyol, Mhispania Joan Garcia, 23, anawindwa na Bayer Leverkusena na Arsenal ambazo zinataka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Timu nyingi zimevutiwa na kiwango cha Garcia alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu ambapo amecheza mechi 29 za michuano yote na kuruhusu mabao 40.


MABOSI wa Chelsea hawana mpango wa kumuuza kiungo wa kimataifa wa Argentina, Enzo Fernandez katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi licha ya Real Madrid kudaiwa kuitaka saini yake. Enzo mwenye umri wa miaka 24, alikuwa akitajwa kwamba huenda akatumika kama sehemu ya mabadilishano ya kumpeleka Aurelien Tchouameni Chelsea kisha yeye akatua Real Madrid.


REAL Madrid imeanza mchakato wa kumsainisha mkataba mpya beki wa kati na timu ya taifa ya Ujerumani,  Antonio Rudiger, 32, wakati ule wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu ujao. Rudiger amekuwa katika rada za vigogo wa Saudi Arabia ambao wamemwekea ofa nono ili akubali kujiunga nao kwa msimu ujao.


INTER Milan haina mpango wa kumsajili kiungo wa Man City na timu ya taifa ya Ubelgiji, Kevin de Bruyne, 33, dirisha lijalo la kiangazi kwa sababu ya umri. De Bruyne kaweka wazi ataondoka mwisho wa msimu huu  baada ya mkataba wake na Man City kumalizika. Mbali ya timu za Ulaya, kuna tetesi anaweza kutua Marekani au Saudi Arabia.