Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal mambo safi

Muktasari:

  • Awali, ilielezwa kwamba Havertz ambaye aliumia tangu Februari, mwaka huu anaweza kuwa nje hadi mwisho wa msimu, lakini kwa sasa maendeleo yake ni mazuri na atarejea mapema zaidi.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kwamba mastaa wake Declan Rice na Bukayo Sako wako freshi na kufichua kuwa huenda Kai Havertz akarejea kabla ya msimu huu kumalizika.

Awali, ilielezwa kwamba Havertz ambaye aliumia tangu Februari, mwaka huu anaweza kuwa nje hadi mwisho wa msimu, lakini kwa sasa maendeleo yake ni mazuri na atarejea mapema zaidi.

Hii imekuwa ni habari njema kwa Arsenal ambayo inapambana kuchukua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia na msimu huu mambo yanaonekana kuwa mazuri kwani ipo hatua ya robo fainali na ilifanikiwa kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Real Madrid.

“Tuna matumaini kwamba tutakuwa naye kabla ya msimu kuisha. Tuone itakuwaje huko mbele. Kila jeraha lina utofauti, lakini Kai anajichunga kwa nidhamu kubwa kwa sababu anataka kurejea uwanjani haraka na timu yetu bora ya madaktari imekuwa ikimsaidia katika hilo,” alisema.

“Unapofika katika hatua za mwisho za kurejea uwanjani, ndipo unaweza kuelewa vyema kama uko karibu au mbali na hatua inayofuata.”

Ilielezwa Alhamisi wiki iliyopita kwamba Declan Rice na Bukayo Saka walipata maumivu madogo katika mechi dhidi ya Real Madrid iliyopigwa Emirates. Hata hivyo, Arteta alitoa taarifa kuhusu nyota hao waliokuwa muhimu kwenye ushindi akisema hawakupata shida kubwa.