Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal kutimua watu ilete wapya

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Majeruhi na viwango vya kupanda na kushuka vimeiathiri kwa namna kubwa Arsenal msimu huu, ambapo sare ya bao 1-1 iliyopata dhidi ya Manchester United uwanjani Old Trafford, Jumapili iliyopita ilihitimisha ndoto za kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu baada ya kujikuta wakiachwa pointi 15 na vinara Liverpool.

LONDON, ENGLAND: NDO hivyo. Maandalizi ya msimu wa 2025/26 kwa Arsenal yameshaanza, ambapo kuna mastaa kadhaa watafunguliwa mlango ili kuleta vyuma vipya.

Majeruhi na viwango vya kupanda na kushuka vimeiathiri kwa namna kubwa Arsenal msimu huu, ambapo sare ya bao 1-1 iliyopata dhidi ya Manchester United uwanjani Old Trafford, Jumapili iliyopita ilihitimisha ndoto za kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu baada ya kujikuta wakiachwa pointi 15 na vinara Liverpool.

Arsenal bado ipo kwenye msako wa ubingwa wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini kwa ishu ya kunyakua taji la ndani hilo limeshaonekana kuwa gumu kwao na sasa wameamua kuweka sawa mipango yao katika kujenga kikosi chao upya kuwa cha kiushindani kwenye dirisha lijalo.

Ripoti zinafichua kwamba Oleksandr Zinchenko, Jorginho, Thomas Partey na Kieran Tierney wanatarajia kufunguliwa mlango wa kutokea dirisha lijalo la majira ya kiangazi, wakati Arsenal ikijaribu kuuza ili kuongeza bajeti itakayomfanya kocha Mikel Arteta kuwa na jeuri kwenye usajili.

 Kwa mujibu wa Transfermarkt, wachezaji hao wanne wanathaminishwa kwa Pauni 55 milioni, lakini watatu kati yao mikataba itakwisha mwisho wa msimu, hivyo Arsenal haitakuwa na fursa ya kupata mkwanja wote huo.

Partey, ambaye mkataba wake utakwisha mwisho wa msimu huu, ndiye pekee anayepata namba kila mechi. Lakini, kiungo huyo wa Ghana ni mmoja ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa akilipwa Pauni 200,000 kwa wiki na atatimiza umri wa miaka 32, Juni.

Kwenye orodha ya mastaa ambao Arsenal inawasaka ni Benjamin Sesko, Viktor Gyokeres, Alexander Isak, Victor Osimhen, Liam Delap, Ollie Watkins, Lautaro Martinez, Nico Williams, Bryan Mbeumo, Antoine Semenyo na Ademola Lookman.