Arsenal kumsajili Dan Bantley

Muktasari:

  • Bantley hakupata nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha West Ham msimu uliopita ambapo alicheza mechiĀ  nane za michuano yote na kuruhusu mabao 14.

ARSENAL inatarajiwa kutuma ofa kwenda Wolves ili kuipata saini ya kipa wa timu hiyo, Dan Bantley, 30, katika dirisha hili ili aende kuwapa changamoto David Raya na Aaron Ramsdale ikiwa ataendelea kuwepo.

Bantley hakupata nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha West Ham msimu uliopita ambapo alicheza mechiĀ  nane za michuano yote na kuruhusu mabao 14.


BAYERN Munich itapata Euro 20 milioni katika mauzo ya straika wa Bologna na Uholanzi, Joshua Zirkzee anayedaiwa kuwa katika rada za Manchester United. Kiasi hicho kinatokana na kipengele ilichokiweka wakati inamuuza Bologna kwamba ikitokea atauzwa tena basi timu hiyo itapata asilimia 50 ya mauzo.

Katika mkataba wa Zirkzee kuna kipengele kinachomruhusu kuondoka ikiwa itatolewa Euro 40 milioni.


IPSWICH inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Everton na Crystal Palace kuwania saini ya kiungo wa AS Monaco, Maghnes Akliouche, ambaye pia kuna uwezekano akatua PSG. Akliouche mwenye umri wa miaka 22 pia anaweza kuendelea kubaki Monaco kwa sababu wawakilishi wake wapo katika mazungumzo na mabosi wa timu hiyo ili kusaini mkataba mpya.


REAL Betis imefikia makubaliano na Leeds United juu ya uwezekano wa kuipata saini ya beki wa timu hiyo, Mhispania Diego llorente, 30, katika dirisha hili. Llorente alikuwa mmoja kati ya mastaa waliofanya vizuri msimu uliopita akiwa na Leeds. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2026. Msimu uliopita alicheza mechi 42 za michuano yote.


ARSENAL ipo tayari kumuuza beki Jakub Kiwior, anayedaiwa kuwasilisha maombi ya kuondoka kwa kuuzwa au kutolewa kwa mkopo. Staa huyu wa kimataifa wa Poland hajawa na wakati mzuri Arsenal tangu ajiunge Januari, mwaka jana akitokea Spezia. Arsenal ipo tayari kumuuza na kama itamtoa kwa mkopo kuwe na kipengele cha lazima cha timu husika kumsajili baada ya mkataba wa mkopo.


KOCHA wa Como iliyopanda Ligi Kuu Italia amewaambia mabosi wa timu yake kwamba anataka huduma ya beki wa kati raia wa Ufaransa, Raphael Varane katika dirisha hili la usajili. Varane ambaye kwa sasa yupo huru baada ya mkataba wake na Man United kumalizika mwisho wa msimu uliopita anawindwa na timu mbalimbali barani Ulaya na nje ya bara hilo.


ROMA imeingilia kati dili la mshambuliaji wa Villarreal, Alexander Sorloth (28), kwenda West Ham katika dirisha hili na inataka kumsajili kwa ajili ya kuziba pengo la Romelu Lukaku aliyekuwa akiitumikia kwa mkopo msimu uliopita. Inaelezwa katika mkataba wa Alexander kuna kipengele ambacho kinamruhusu kuondoka ikiwa kuna timu itatoa Pauni 32 milioni.