Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal kumpata Isak ichimbe kwelikweli

Muktasari:

  • Newcastle United haina mpango wa kumuuza straika wao huyo na badala yake inataka kujenga timu kuzungumka mkali huyo. Na kama itaamua kumpiga bei, basi inaweza kuwa mara mbili ya ada ya Pauni 82.9 milioni ambayo imekuwa ikiripotiwa.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imekwaa kisiki kwenye matumaini yao ya kumfanya Alexander Isak kuwa Namba 9 wao mpya.

Newcastle United haina mpango wa kumuuza straika wao huyo na badala yake inataka kujenga timu kuzungumka mkali huyo. Na kama itaamua kumpiga bei, basi inaweza kuwa mara mbili ya ada ya Pauni 82.9 milioni ambayo imekuwa ikiripotiwa.

Jambo hilo litamfanya Isak kuwa mchezaji ghali namba mbili duniani - nyuma ya ada iliyowahi kulipwa na Paris Saint-Germain ya Pauni 198 milioni kumnasa Neymar kutoka Barcelona 2017 na juu ya ada ya Pauni 163 milioni iliyolipwa pia na PSG huko Monaco kumchukua Kylian Mbappe 2018.

Isak, 25, amekuwa mmoja wa washambuliaji matata kabisa tangu aliponaswa kwa ada ya Pauni 63 milioni kutoka Real Sociedad mwaka 2022. Amekuwa mchezaji wa kwanza wa Newcastle United tangu gwiji Alan Shearer miongo miwili iliyopita kufunga mabao 20 kwenye Ligi Kuu England alipofanya hivyo msimu uliopita.

Msimu huu tayari ameshafunga mabao 17 kwenye ligi na huenda akaandika zama mpya kwenye kikosi hicho kwa kuipa Newcastle taji lao la kwanza baada ya miaka 70 endapo kama itashinda kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Ligi itakayofanyika mwezi ujao.

Hata hivyo, kiwango chake bora huko St James' Park kimezivutia timu nyingi na kuhitaji saini yake, ikiwamo Arsenal, ambayo ipo kwenye msako wa kutafuta straika wa kuja kuwapa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Timu nyingine zinazomtaka Isak ni Liverpool na Chelsea, huku mkataba wake wa huko Newcastle unaomshuhudia akilipwa Pauni 130,000 kwa wiki utafika tamati 2028.


USAJILI GHALI WA MARA MOJA DUNIANI NI HUU

1.Neymar (Barc -PSG, Pauni 198milioni, 2017)

2.Kylian Mbappe (Monaco - PSG, Pauni 163milioni, 2018)

3.Philippe Coutinho (Liverpool - Barca, Pauni 142milioni, 2018)

4.Ousmane Dembele (Dortmund - Barca, Pauni 135.5milioni, 2017)

5.Moises Caicedo (Brighton - Chelsea, Pauni 115milioni, 2023

6.Jude Bellingham (Dortmund - Real Madrid, Pauni 114milioni, 2023)

7.Joao Felix (Benfica - Atletico Madrid, Pauni 112.9milioni, 2019)

8.Enzo Fernandez (Benfica - Chelsea, Pauni 107milioni, 2023)

9.Antoine Griezmann (Atletico - Barca, Pauni 107milioni, 2019)

10.Declan Rice (West Ham - Arsenal, Pauni 105milioni, 2023)