Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal kufanya mabadiliko makubwa

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Jioni ya Jumamosi ya wiki iliyopita, matumaini ya Arsenal ya kushinda Ligi Kuu yalipata pigo jingine baada ya kutoka sare na Everton. 

LONDON, ENGLAND: ARSENAL wametajwa kuwa na mpango wa kufanya maboresho makubwa katika kikosi chao kwa kusajili wachezaji wanne katika dirisha la uhamisho la majira ya kiangazi mwaka huu.

Jioni ya Jumamosi ya wiki iliyopita, matumaini ya Arsenal ya kushinda Ligi Kuu yalipata pigo jingine baada ya kutoka sare na Everton. 

Arteta sasa atakuwa na kibarua kingine mbele ya Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa ikiwa ni mashindano ambayo wanaweza kufanya chochote kutokana na hali ilivyo.

Akizungumza na TNT Sports, mtaalamu wa habari za usajili, Guillem Balague alisema: "Arsenal itabidi wawe makini na wachezaji wao watano watakaokuwa wanaelekea kumaliza mikataba yao, na itabidi wasajili wachezaji watatu au wanne watakaokwenda moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza. 

"Naweza kusema wanahitaji winga wa kushoto, mshambuliaji wa kati, na kiungo wa kati. Tumesikia majina kama Martin Zubimendi, Viktor Gyokeres pia Benjamin Sesko na Nico Williams, haya ni majina wanayojaribu kuyasajili." 

Aliongeza: "Mkurugenzi wa michezo, Berta itabidi awe makini. Arsenal hawapo hapa kwa nia ya kutumia Pauni 200 milioni au Pauni 300 milioni kwa mchezaji yeyote, inahitaji umakini na jicho kali kusajili wachezaji watakaoisaidia.

"Hawawezi kutumia pesa nyingi kabla ya kuanza kuuza, hivyo kutakuwa na mambo mengi yanaendelea ifikapo dirisha hilo."

Baada ya kumenyana na Madrid katika Ligi ya Mabingwa, Arsenal watarudi kwenye Ligi Kuu Jumamosi ijayo watakapokutana na Brentford kwenye Uwanja wa Emirates.