Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal ilivyorudi Ulaya na utamu wake

LONDON, ENGLAND. ARSENAL imemaliza kiu ya kusubiri muda mrefu kurudi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na imerudi kibabe baada ya kuichapa PSV 4-0 uwanjani Emirates, Jumatano iliyopita.

Hilo limekuja baada ya subira ya miaka sita kuiona Arsenal kwenye michuano hiyo mikubwa ya ngazi ya klabu Ulaya, ilipokuwa ikijitafuta baada ya kucheza kwa miaka 19 mfululizo ilipokuwa chini ya Arsene Wenger.

Baada ya kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Manchester City kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita, Arsenal yenye vijana wengi wenye njaa ya mafanikio, ilirudi kwa kishindo kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kumbabua bao nyingi mpinzani wake.

Bukayo Saka, Leandro Trossard, Gabriel Jesus na Martin Odegaard wote walitikisa nyavu kwenye mechi hiyo dhidi ya vijana wa Eredivisie, ambao walikwenda Emirates wakiwa na rekodi ya asilimia 100 ya ushindi kwenye ligi yao ya Uholanzi. Kilichowakuta, wamejua hawajui.

Wakati Arsenal ikirejea kibabe kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, haya hapa mambo 10 yaliyovutia kwenye mechi yao hiyo ya kwanza walipowafundisha mpira PSV.

Kila mtu kwenye ile safu ya washambuliaji watatu amefunga bao, huku Saka na Trossard wakiasisti pia.

Hii ni mara ya kwanza kwenye historia ya Arsenal kushuhudia wachezaji wake wawili wanaocheza kwa mara ya kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufunga mabao (Saka na Trossard).

Arsenal ilimiliki mpira kwa asilimia 59, imepiga mashuti 17 na kufunga mara nne. Waliishika mechi.

Wachezaji tisa kati ya 10 waliohusika kwenye kutengeneza mashambulizi kwenye mechi hiyo, walikuwa wa Arsenal, huku beki Ben White akihusika mara kadhaa kupandisha mashambulizi.

Arsenal ilikuwa moto kipindi cha kwanza, ikifunga bao lake la haraka zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati Saka alipofunga dakika ya nane. Walilenga golini mashuti saba kati ya nane waliyopiga kipindi cha kwanza.

Gabriel Jesus sasa amefikisha mabao 21 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya mechi 39. Mbrazili huyo amefunga nusu ya mabao hayo katika mechi ambazo alianzishwa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Arsenal kuanza msimu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi katika kipindi cha miaka 10, tangu ilipofanya hivyo msimu wa 2013-14 dhidi ya Marseille. Pia ni ushindi wao mkubwa tangu waliposhinda 6-0 dhidi ya Braga msimu wa 2010-11.

Mchezaji bora wa mechi, Odegaard alifunga bao moja, alipiga pasi 64 sahihi, ambazo ndizo zilizokuwa nyingi zaidi katika mechi hiyo, huku akifanya majaribio ya kukokota mpira na kupita wapinzani mara tatu.

Wachezaji wote walioitumikia Arsenal kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2016-17 wote wameondoka. Granit Xhaka alikuwa mchezaji wa mwisho wa Arsenal kuichezea timu hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati walipochapwa 5-1 na Bayern Munich, ambaye ameachana na maisha ya Emirates mwaka huu.

Kwenye kikosi cha Arsenal kilichoanza, wachezaji saba walikuwa wakicheza mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ni Oleksandr Zinchenko, Kai Havertz, Jesus na Odegaard pekee ndio waliokuwa wamewahi kucheza michuano hiyo huko nyuma, walipokuwa na timu nyingine kabla ya kutua Emirates.