Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Darwin Nunez kuna jambo

NUNEZ Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anamwangalia mchezaji huyu kama mmoja kati ya washambuliaji anaohitaji kupata huduma zao katika dirisha lijalo.

LIVERPOOL ipo tayari kumuuza mshambuliaji wake raia wa Uruguay, Darwin Nunez katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa timu za ndani au nje ya England.

Inaelezwa, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anamwangalia mchezaji huyu kama mmoja kati ya washambuliaji anaohitaji kupata huduma zao katika dirisha lijalo.

Kati ya maeneo ambayo Arsenal imekuwa ikihitaji kuyafanyia maboresho ni hili ambalo limekuwa na upungufu kutokana na majeraha yaliyowahi kuwakumba washambuliaji hao.

Msimu huu kocha huyo alilazimika kumtumia Kai Havertz kama straika kabla hajaumia na kumfanya aumize kichwa zaidi.

Mkataba wa Nunez unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu huu amecheza mechi 39 za michuano yote na kufunga mabao saba.

Liverpool inataka kumuuza kwa sababu haonekani kuwa katika mipango ya kocha Arne Slot kuelekea msimu ujao na hiyo ni kwa sababu haridhishwi na kiwango chake.


Marc Guehi

LIVERPOOL inakaribia kuzipiku Chelsea na Newcastle United kwenye mchakato wa kuiwania saini ya  kiungo wa Crystal Palace, Marc Guehi, mwenye umri wa miaka 24, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Guehi ambaye ni miongoni mwa mabeki tegemeo katika kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya England, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.



William Saliba

LICHA ya kufaiwa kuwa na mpango wa kuendelea kusalia Arsenal, vigogo wa Real Madrid  wamepanga kutuma ofa kwenda kwa washika mitutu hao ili kumsajili beki wa timu hiyo na Ufaransa, William Saliba, mwenye umri wa miaka 23,  katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Fundi huyu ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2027, msimu huu amecheza mechi 38 za michuano yote.


Jonathan David


MANCHESTER United, Liverpool na West Ham zimeanza vita ya kuiwania saini ya  mshambuliaji wa Lille na Canada Jonathan David mwenye umri wa miaka 25, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Hata hivyo, huduma ya fundi huyu pia inawindwa na timu nyingine kutoka Italia na Hispania ambazo ni  Barcelona, Juventus na Inter Milan.


Semih Kilicsoy

NEWCASTLE United na Aston Villa ndio zinaongoza katika vita ya kuiwania saini ya  mshambuliaji wa Besiktas, Semih Kilicsoy, 19, kuelekea dirisha lijalo.

Fundi huyu ambaye pia anahitajika na  Fulham, Everton na Nottingham Forest, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Jobe Bellingham

SUNDERLAND inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 20 milioni ili kumuuza kiungo wao Jobe Bellingham, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Jobe ambaye ni mdogo wake Jude Bellingham ameonyesha kiwango bora akiwa na Sunderland kiasi cha timu nyingi kuonyesha nia ya kumsajili.

Miongoni mwa timu zinazopigana vikumbo ili kumpata ni pamoja na Borussia Dortmund, Chelsea, Crystal Palace na Tottenham.


Timo Werner

STRAIKA wa RB Leipzig, Timo Werner, 29, ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo Tottenham, huenda akaamua kwenda New York Bulls kwa mkopo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya  Tottenham kuwaambia wawakilishi wake kwamba hawatomsainisha mkataba wa kudumu wa kuendelea kusalia timu hiyo baada ya kocha kutoridhishwa kiwango chake. Msimu huu amecheza mechi 27 za michuano yote na kufunga bao moja.


Christian Pulisic

MSHAMBULIAJI raia wa Marekani, Christian Pulisic, amesisitiza kwamba anataka kubaki AC Milan licha ya tetesi zinazodai kuwa huenda akaondoka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya timu nyingi kuonyesha tamaa ya kumsajili kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu msimu uliopita.

Moja ya mambo yanayodaiwa kuwa huenda yakachangia kumshawishi aondoke ni ikiwa Milan itashindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.