Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea FC yashikwa pabaya Uefa

Muktasari:

  • The Blues imeshatumia zaidi ya Pauni 160 milioni kwenye usajili wa Delap, Pedro, kinda wa Kibrazili Willian Estevao na Jamie Gittens aliyenaswa kutoka Borussia Dortmund kwa dili la Pauni 52 milioni.

LONDON, ENGLAND: KIMENUKA. Chelsea huenda ikapigwa pini kuwatumia mastaa wake wapya Liam Delap, Joao Pedro na wengine itakaowasajili dirisha hili kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

The Blues imeshatumia zaidi ya Pauni 160 milioni kwenye usajili wa Delap, Pedro, kinda wa Kibrazili Willian Estevao na Jamie Gittens aliyenaswa kutoka Borussia Dortmund kwa dili la Pauni 52 milioni.

Lakini, kama Chelsea itashindwa kuweka sawa vitabu vyake vya hesabu kwa kuuza au kutoa kwa mkopo wachezaji kabla ya dirisha kufungwa, kwa mujibu wa adhabu za Uefa kwa kukiuka matumizi itazuiwa kuwatumia wachezaji hao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Na hilo ndio maana beki Trevoh Chalobah anaweza kupigwa bei kwenye dirisha hili. Hata hivyo, ada ya Pauni 40 milioni kwenye mauzo ya Chalobah bado haitoshi kuziba pengo la pesa zilizotumika kusajili.

Uefa wiki iliyopita iliipiga Chelsea faini ya Pauni 27 milioni na huenda ikapanda hadi Pauni 52 milioni kutokana na kukiuka matumizi kwa maana ya kipato chao hakiendani na matumizi.

Na kwenye hilo, The Blues ilikubali kwamba haitawajumuisha wachezaji wapya kwenye kikosi cha mastaa 25 watakaoruhusiwa kucheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Gharama ya mchezaji kwa mwaka inakokotolewa na kujumlisha mshahara wake na thamani ya ada. Kwa mfano, straika Delap alijiunga na Chelsea akitokea Ipswich kwa ada ya Pauni 30 milioni na kusainishwa mkataba wa miaka sita. Lakini, kanuni za Uefa, kikokotoo chake kinafanyika kwa kuzingatia miaka mitano. Hivyo, gharama halisi ya Delap kwa msimu ujao, itakuwa Pauni 30 milioni kwa kugawanya kwa miaka mitano, hivyo inakuwa Pauni 6 milioni.

Kama straika huyo mshahara wake ni Pauni 100,000 kwa wiki, hiyo ni sawa na Pauni 5.2 milioni kwa mwaka, jambo litakalofanya thamani ya mchezaji Delap ni Pauni 11.2 milioni.

Kama Chelsea inataka kumtumia kwenye Ligi ya Mabingw Ulaya, inapaswa kutafuta mchezaji mwenye thamani ya Pauni 11.2 milioni kwenye kikosi chao na kumwondoa kwenye kikosi.

Thamani ya mchezaji anayeondoka, inakokotolewa kwa kujumlisha mshahara wake na faida itakayopatikana kwenye mauzo yake. Na ndiyo maana Chalobah anawekwa sokoni kwa sababu faida yake ni kubwa kutokana na kutokea kwenye akademia ya klabu hiyo. Kitu kama hicho ndicho kilichofanyika kwenye mauzo ya Mason Mount na Conor Gallagher kwamba ni wachezaji wa kutoka kwenye akademia, hivyo faida yao ilikuwa na faida kubwa kwa timu.

Kama Chalobah atauzwa kwa Pauni 40 milioni, kujumlisha pesa itakayookolewa kutoka kwenye mshahara wake, zitaweza kuziba pengo la matumizi yaliyofanyika kwa Delap, Joao Pedro na wengine wachache - lakini si wachezaji wote watakaosajiliwa na The Blues kwenye dirisha hili.

Lakini, kama Chelsea inataka kumuuza mchezaji kama kipa Robert Sanchez, hesabu zake zitakuwa tofauti. Sanchez alitua Chelsea akitokea Brighton kwa Pauni 25 milioni miaka miwili iliyopita. Thamani yake ya miaka hiyo miwili ni Pauni 5 milioni (Pauni 25 milioni gawa kwa 5) kufanya gharama yake kuwa Pauni 10 milioni. Thamani ya Sanchez ni Pauni 15 milioni (Pauni 25milioni toa Pauni 10 milioni) hivyo, Chelsea hivyo, Chelsea itahitaji kumuuza kwa pesa nyingi sana ili kuziba pengo hilo.

Kwenye kikosi cha wachezaji 25 wa Chelsea waliocheza kwenye Europa Conference League, mchezaji pekee mkubwa aliyeondoka ni Jadon Sancho, aliyekuwa kwa mkopo kwenye timu hiyo. Chelsea ilikuwa inamlipa Sancho nusu ya mshahara wake, Pauni 150,000 kwa wiki na timu yake ya Manchester United ikilipa salio lililobaki la Pauni 150,000 kwa wiki, kukamilisha Pauni 300,000 kwa wiki.

Kwa maana hiyo, Chelsea inahitaji kuuza wachezaji ili kutumia mastaa wapya kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao.