Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arne Slot aanza kuwaza msimu mpya

SLOT Pict

Muktasari:

  • Slot anazungumzia michuano ya Kombe la Dunia la Klabu kwamba linaloshirikisha baadhi ya timu litazifanya timu hizo kuwa kwenye wakati mgumu kabla ya msimu mpya kuanza kwa sababu wachezaji wao watakuwa wamechoka.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot anaamini kikosi chake kitakuwa na faida kubwa kwenye mchakamchaka wa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao kutokana na wapinzani kuwa na mechi za ziada zinazowachosha wachezaji wao.

Slot anazungumzia michuano ya Kombe la Dunia la Klabu kwamba linaloshirikisha baadhi ya timu litazifanya timu hizo kuwa kwenye wakati mgumu kabla ya msimu mpya kuanza kwa sababu wachezaji wao watakuwa wamechoka.

Manchester City na Chelsea kutoka kwenye Ligi Kuu England ndizo zitakazokwenda kushiriki fainali hizo za Fifa, ambazo zitafanyika kwa zaidi ya mwezi mmoja huko Marekani kuanzia katikati ya Juni.

Slot alisema: "Kila mtu ana maoni yake - na nadhani tulio wengi kwenye soka tumekuwa na maoni yanayofanana kuhusu michuano hii. Zinapochezwa ni wazi tunaona kila mmoja angepenga kushiriki michuano hiyo mikubwa. Lakini, wakati sahihi wa kujibu hilo ni baada ya michuano. Lakini, kwa sasa, nane ya 10 ya watu wanaofanya kazi kwenye biashara hii ya soka bado hawaoni muhimu wa michuano hii kutokana na msimu mrefu tuliokuwa nao. Pengine, inaweza kuwa 10 kwa 10.

"Sidhani kama ni afya kwa wachezaji kwa sababu watakuwa na wiki moja tu ya kupumzika kwenda kwenye michuano hiyo, kisha watakuwa na wiki moja nyingine kabla ya msimu wa Ligi Kuu England kuanza.

"Hilo haliwezi kuwa zuri kwa afya za wachezaji. Kama itakuwa ni michuano mzuri bado itanyanyua wachezaji kuelekea msimu ujao. Niliwahi kuwa Feyenoord ambako tulikuwa na mechi za kufuzu kucheza Conference League na mara nyingi zilikuwa zikifanyika katika kipindi cha mapumziko ya msimu. Ngoja tuone itakavyokuwa, hizi timu zitakuwa na wakati mgumu kwa wachezaji wake kukosa muda wa kutosha wa kupumzika."