Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Antonio Conte kuipiga kibuti Napoli

CONTE Pict

Muktasari:

  • Conte, 55, aliiongoza Napoli kunyakua taji la nne la Scudetto wakati walipoibwaga Inter Milan kwenye vita ya ubingwa msimu huu na kubeba taji kwa tofauti ya pointi moja.

NAPLES, ITALIA: KOCHA, Antonio Conte amepanga kuachana na Napoli kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi licha ya kuiongoza klabu hiyo kushinda taji la Serie A msimu huu, imeelezwa.

Conte, 55, aliiongoza Napoli kunyakua taji la nne la Scudetto wakati walipoibwaga Inter Milan kwenye vita ya ubingwa msimu huu na kubeba taji kwa tofauti ya pointi moja.

Kocha huyo Mtaliano, ambaye alijiunga na klabu hiyo wakati wa dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, ana mkataba kwenye kikosi cha Napoli hadi 2027.

Lakini, sasa anajiandaa kuachana na mabingwa hao wa Italia miaka miwili kabla ya mkataba wake kwisha.

Kwa mujibu wa Gianluca Di Marzio, Conte amepanga kuzungumza na mabosi wa Napoli na kuna wasiwasi mkubwa kwamba kikao hicho kitahitimishwa kwa kocha huyo kuondoka.

Rais wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis anataka kupata mafanikio makubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na Conte hatazamwi kama mtu wa kwenda kuiongoza timu hiyo.

Na badala yake, De Laurentiis ameripotiwa kuanza kufungua milango ya kumbadili kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Tottenham, huku ikielezwa Massimiliano Allegri anaweza kupewa mikoba ya kumrithi Conte.

Ripoti zinafichua kwamba Conte na De Laurentiis wamekuwa na uhusiano wenye shaka kwa kipindi cha karibuni baada ya kupishana kwenye masuala ya usajili na vifaa vya mazoezi.

Moja ya usajili wake, Conte kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana ndiye aliyefanya mambo kuipa Napoli ubingwa huo wa Serie A. Staa huyo aliyesajiliwa na Conte ni Scott McTominay, ambaye alichaguliwa pia kuwa Mchezaji Bora wa Msimu wa Serie A. McTominay alijiunga na Napoli kwa ada ya Pauni 25 milioni.