Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Staa NBA ataja timu mpya ya Ronaldo

Muktasari:

  • Hatima ya Ronaldo imekuwa ikigonga vichwa vya habari vingi baada ya nyota huyo wa Ureno kuashiria kuwa anaweza kuondoka na tetesi kudai anataka kujiunga na timu itakayomwezesha kushiriki michuano ya  Klabu Bingwa Dunia.

RIYADH, SAUDI ARABIA: STAA wa NBA Giannis Antetokounmpo anayeichezea,  Milwaukee Bucks na timu ya taifa ya Kikapu ya  Ugiriki ametoa ushauri wa uhamisho kwa  mshambuliaji wa Al Nassr na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo baada  ya tetesi kwamba anaweza akaondoka Saudia katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hatima ya Ronaldo imekuwa ikigonga vichwa vya habari vingi baada ya nyota huyo wa Ureno kuashiria kuwa anaweza kuondoka na tetesi kudai anataka kujiunga na timu itakayomwezesha kushiriki michuano ya  Klabu Bingwa Dunia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 sasa anahusishwa na klabu mbalimbali na mashabiki wengi wanasubiri kuona hatua yake inayofuata.

Ronaldo anaripotiwa kutakiwa na wapinzani wa Al-Nassr kwenye Ligi Kuu ya Saudi Arabia, Al-Hilal, ambao wanataka kuingiza jina kubwa baada ya kuondoka Neymar.

Al-Hilal pia wanatarajiwa kushiriki Kombe la Dunia la Klabu, jambo ambalo linaweza kumvutia Ronaldo analihitaji kwa sasa.

Giannis,  ambaye tayari ameonyesha wazi jinsi anavyomkubali Ronaldo, alitoa mtazamo wake juu ya wapi angependa kuona fundi huyo akienda.

Aliandika kwenye Instagram: “Njoo ucheze Ugiriki. Olympiacos, Panathinaikos, AEK, au PAOK. Sijali, chochote unachotaka.”

Baadhi ya ripoti zilimhusisha staa huyu na timu za Brazil ikiwemo Flamengo lakini timu hiyo imekanusha kutaka kumsajili.