Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim: Ratcliffe ametupa mzuka

Muktasari:

  • Mmiliki mwenza huyo wa Man United, bilionea Ratcliffe alisema kwenye mahojiano aliyofanya wakati wa mapumziko ya ligi kupisha mechi za timu za taifa Oktoba kwamba ana imani kubwa na kocha huyo Mreno na ataanza kumhukumu baada ya miaka mitatu.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA mkuu wa Manchester United, Ruben Amorim anaamini maneno ya bilionea Sir Jim Ratcliffe aliyosema kwamba ana imani na kocha huyo umeamsha morali mkubwa katika kikosi hicho cha Old Trafford.

Mmiliki mwenza huyo wa Man United, bilionea Ratcliffe alisema kwenye mahojiano aliyofanya wakati wa mapumziko ya ligi kupisha mechi za timu za taifa Oktoba kwamba ana imani kubwa na kocha huyo Mreno na ataanza kumhukumu baada ya miaka mitatu.

Na sasa, Amorim ndio kwanza yupo kwenye mwaka wake wa kwanza kwenye kikosi hicho cha Man United, hivyo bado kuna safari ndefu katika kutimiza malengo ya timu hiyo.

Amorim alikuwa kwenye presha kubwa juu ya usalama wa kibarua chake baada ya kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Brentford mwishoni mwa Septemba, lakini tangu wakati huo, Man United imeshinda mechi tatu mfululizo na kutoka sare mbili katika mechi tano zilizopita.

Na sasa kocha huyo wa zamani wa Sporting Lisbon anaamini maneno ya Ratcliffe aliyosema mwezi uliopita yalishusha presha ndani ya klabu na mambo yameanza upya.

Amorim alisema: “Kama unakumbuka yale mahojiano ya Jim, ilituliza sana hali ya mambo kwenye klabu. Zile kelele kwenye klabu zimebadilika sana, hakika yalikuwa maneno muhimu kwa timu na kwangu binafsi. Imekuwa na faida kubwa, si kwa namna ninavyofanya kazi, bali ni namna watu wanavyoitazama timu yetu kwa sasa. Yalikuwa maneno mazuri kwetu.”

Ilikuwa mapema Oktoba wakati Ratcliffe aliposema Amorim atakuwa na ulazima wa kuonyesha ubora wake kwa kipindi cha kuanzia miaka mitatu kwamba muda huo atakuwa kwenye wakati mzuri wa kuwa kocha mahiri wa Man United.

Amorim alisema kwa kipindi cha miezi 12 kwenye timu hiyo anajiona ni mwenye bahati kubwa kutokana na kuendelea kubaki kazini.


USAJILI ULIOFANYWA NA AMORIM KWENYE DIRISHA LILILOPITA

Bryan Mbeumo – Pauni 71 milioni

Matheus Cunha – Pauni 62.5 milioni

Diego Leon – Pauni 7 milioni

Benjamin Sesko – Pauni 74 milioni

Senne Lammens – Pauni 18 milioni

JUMLA – Pauni 232.5 milioni