Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Semenyo anachotaka ni Arsenal tu basi

Muktasari:

  • Semenyo, 25, atafunguliwa mlango wa kutokea kwa ada ya Pauni 65 milioni kwenye dirisha la uhamisho wa Januari baada ya mkataba wake aliosaini miezi minne iliyopita kuwekewa kipengele hicho kinachotajwa kiasi hicho cha bei.

BOURNEMOUTH, ENGLAND: STAA wa Bournemouth, Antoine Semenyo amefunguka akifichua kwamba ni Arsenal tu ndiko anakotamani kwenda kukipiga baada ya maisha ya Vitality Stadium kufika ukomo.

Semenyo, 25, atafunguliwa mlango wa kutokea kwa ada ya Pauni 65 milioni kwenye dirisha la uhamisho wa Januari baada ya mkataba wake aliosaini miezi minne iliyopita kuwekewa kipengele hicho kinachotajwa kiasi hicho cha bei.

Bournemouth haitamzuia mshambuliaji huyo endapo kama kutakuwa na timu itakayokuwa tayari kulipia kiwango hicho cha pesa ndani ya wiki mbili za kwanza katika dirisha la Januari na kama mchezaji mwenyewe atataka kuondoka.

Semenyo amekuwa mmoja wa wachezaji wanaocheza vizuri sana kwenye Ligi Kuu England msimu huu, akifunga mabao sita na kuasisti mara tatu katika mechi 12.

Mzaliwa huyo wa London, anayeitumikia Ghana kwenye soka la kimataifa aliwahi kuhusishwa pia na timu za Manchester United, Liverpool na Tottenham.

Kocha wa Man United, Ruben Amorim aliripotiwa kukutana na Semenyo mwishoni mwa msimu uliopita kabla ya mchezaji huyo kukataa ofa hiyo ya kwenda Old Trafford na kusaini dili jipya.

Staa huyo wa zamani wa Bristol City ndoto zake ni kwenda kukipiga Emirates, wakati aliposema: "Mimi ni shabiki wa Arsenal. Ni kitu kizuri kucheza dhidi ya Arsenal, timu ambayo nimekuwa nikiitazama kwa maisha yangu yote na nataka kucheza timu kubwa pia. Ili hilo kutimia, nahitajika kuonyesha hilo."

Semenyo aliongeza: "Timu yoyote inayocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europa League hilo ndio lengo. Nafahamu hilo haliwezi kutokea kwa kubofya tu kwa kidole, bali linahitaji muda. Linahitaji kufunga mabao, linahitaji kucheza kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu. Naendelea kupambana, hilo ndilo lipo kwenye akili yangu."