Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim: Ni zali tu kubaki Manchester United

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Ni hivi karibuni tu msimu huu ndipo kocha huyo Mreno aliposhuhudia timu yake ya Man United ikishinda kwenye mechi tatu mfululizo kwenye Ligi Kuu England na kuonekana walau timu yake inaanza kujipata taratibu.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA, Ruben Amorim amekiri kuwa ni mwenye bahati kuendelea kuwapo kwenye benchi la ufundi la Manchester United kutokana na matokeo ya hovyo iliyopata timu hiyo hasa kwenye mwaka wake wa kwanza alipopoteza fainali ya Europa League dhidi ya Tottenham.

Ni hivi karibuni tu msimu huu ndipo kocha huyo Mreno aliposhuhudia timu yake ya Man United ikishinda kwenye mechi tatu mfululizo kwenye Ligi Kuu England na kuonekana walau timu yake inaanza kujipata taratibu.

Baada ya mechi hizo tatu za ushindi mfululizo, Man United ilishindwa kupata ushindi kwenye mechi mbili zilizopita, ilipotoka sare dhidi ya Nottingham Forest na Spurs.

Amorim alikuwa kwenye wakati mgumu kutokana na nafasi iliyomaliza Man United kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita, namba 15. Kichapo kwenye fainali ya Europa League kiliibua wasiwasi mkubwa juu ya usalama wa kibarua chake huko Old Trafford, lakini mabosi hawakuchoka kumsapoti.

Kwa kipindi chote hicho kocha huyo wa zamani wa Sporting Lisbon aling’ang’ania kutumia falsafa zake licha ya kukosolewa sana na wachambuzi kwamba haiwezi kufanya kazi kwenye kikosi hicho cha Man United na hasa kwenye EPL.

AMO 01

Na kuhusu fainali ya Europa League, Amorim alisema kikosi chake cha Man United kilistahili kushinda katika mechi ile iliyofanyika Bilbao.

Amorim alisema: “Nina bahati sana kuendelea kuwa hapa. Na ni kitu kizuri kufahamika kwamba ni jinsi gani nilivyo na bahati kupata nafasi hii. Kama uliona ile mechi, nadhani tulistahili kushinda. Lakini, ndo hivyo. Ni ngumu kuona kocha aliyeshinda lile kombe la Ulaya ndiye aliyeondolewa na aliyepoteza amebaki.”

Mmiliki mwenza wa Man United, bilionea Sir Jim Ratcliffe hivi karibuni aliibuka na kusema kwamba atampatia Amorim kipindi kisichopungua miaka mitatu ili kukifuma kikosi hicho kurudi kwenye ubora wake. Kauli ya tajiri huyo imezima midomo yote ya watu waliokuwa wakitaka atimuliwe.