Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim ajibu tuhuma za Cristiano Ronaldo

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Ronaldo alimwambia Piers Morgan kwenye mahojiano kuwa Man United haiko kwenye njia sahihi, kutokana na kuwa mikononi mwa kocha Amorim, aliyerithi mikoba ya Erick Ten Hag mwaka 2024.

Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim amejibu ukosoaji uliotolewa mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo, Cristiano Ronaldo, mapema wiki hii. 

Ronaldo alimwambia Piers Morgan kwenye mahojiano kuwa Man United haiko kwenye njia sahihi, kutokana na kuwa mikononi mwa kocha Amorim, aliyerithi mikoba ya Erick Ten Hag mwaka 2024.

Katika mahojiano hayo, Ronaldo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, pia alionya kuwa Amorim hatafanya miujiza kwa kuinusuru Man United, kutokana na mambo yanavyoendelea kwenye kikosi chake, ambacho hakijaanza vizuri msimu huu.

Akizungumzia tuhuma hizo, katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mechi ya Ligi ya England dhidi ya Tottenham Hotspur kesho Jumamosi Novemba 8, 2025, Amorim amesema, hakuna haja ya kuangalia nyuma na kuzungumzia yaliyopita, kwa sasa kila shabiki wa Man United na Ronaldo wanapaswa kuangalia mbele.

"Bila shaka, yeye (Ronaldo) ana athari kubwa kwa kila kitu alichosema," Amorim amesema.

"Tunachohitaji kuzingatia ni kesho. Tunajua kwamba sisi, kama klabu, tumefanya makossa mengi hapo nyuma, lakini tunajaribu kubadilisha hilo, kwa kufanya mazuri kuanzia sasa na kuendelea kwa siku zijazo.

"Kwa sasa hatutakiwi kujadili wala kuzungumzia yaliyopita. Tuzingatie tunafanya nini kwa lengo la kusaka mafanikio ya ndani ya uwanja.

"Tunabadilisha mambo mengi kwenye muundo, jinsi tunavyofanya mambo, jinsi tunavyotaka wachezaji wafanye. Tunafanya hivyo na tunaboresha.

"Mafanikio ya wachezaji ni tofauti kwenye kikosi kwa sasa," ameongeza.

"Pia tuna wachezaji walicheza mwaka jana. Lakini sisi ni timu bora. Tunaelewa nini tunachokifanya kwa sasa. Tuna uhakika zaidi," amesema kocha huyo mwenye umri wa miaka 40.