Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim ni Mourinho mpya?

Muktasari:

  • Kocha huyo wa Manchester United alishuhudia kikosi chake kikicheza kwenye kiwango bora kabisa tangu alipochukua mikoba ya Erik ten Hag mapema msimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA, Ruben Amorim amepita kwenye nyayo za shujaa wake Jose Mourinho na kufanikiwa kutibua mipango ya Arsenal kwa kuibana na kutoka nayo sare kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, huku akidai alitaka kushinda mechi.

Kocha huyo wa Manchester United alishuhudia kikosi chake kikicheza kwenye kiwango bora kabisa tangu alipochukua mikoba ya Erik ten Hag mapema msimu huu.

Amorim, 40, amekuwa hana vitu vingi vya kushangilia tangu alipoteuliwa kuwa kocha wa Man United, Novemba mwaka jana. Lakini, sare 1-1 dhidi ya Arsenal uwanjani Old Trafford yalikuwa matokeo mazuri. Katika mchezo huo, Man United ilitangulia kwa bao la friikiki la Bruno Fernandes.

Shuti matata la Declan Rice kwenye dakika za mwisho za kipindi cha pili ziliisaidia Arsenal kusawazisha, lakini matokeo hayo yamewaondoa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

Arsenal ya Mikel Arteta ilikaa na mpira muda mwingi kwenye mechi hiyo, lakini ilishindwa kutengeneza nafasi muhimu za kufunga. Lakini, Man United kwa upande wao, walitengeneza nafasi za hatari nyingi zaidi na kwamba hawakuwa tu na bahati huku kipa wa Arsenal, David Raya akifanya kazi kubwa ya kuwagomea Noussair Mazraoui, Joshua Zirkzee na Fernandes kupeleka majanga zaidi huko Emirates.

Kwenye mechi hiyo, Man United ilionekana kufurahia kukaa kwenye nusu yao na kunyonya mashambulizi ya Arsenal. Kwa timu nzima ya Man United, Alejandro Garnacho peke yake ndiye aliyekuwa anatamba kwenye nusu ya upande wa goli la Arsenal kwa dakika zote 90.

Lakini, kwa kulinganisha na Arsenal wao wachezaji wao wote walikuwa wakitamba kwenye nusu ya goli la Man United isipokuwa Gabriel Magalhaes na William Saliba tu. Lakini, mbinu za Amorim ziliifanya Arsenal kuacha mapengo makubwa nyuma ya mabeki wao na ndipo hapo walipita kushambulia.

Na kwenye hilo, mara kadhaa Man United ilikaribia kufunga mabao kama si kipa Raya kufanya kazi ya ziada, ikiwamo kumgomea Fernandes kwenye dakika za mwisho za mchezo huo, alipookoa shuti, kabla ya kwenda kuondoa mpira kwenye mstari wa goli lake.

Akizungumza baada ya mechi, Amorim alisema huwa hapendi kucheza kwa kukabia chini, alifanya hivyo makusudi kwa sababu alihitaji matokeo mazuri kwenye mechi hiyo, aliposema: "Nadhani tulifanya vizuri. Ipo wazi hatupendi kucheza staili ile ya kukabia chini na kumpa mpinzani muda mwingi wa kuwa na mpira. Lakini, kwa mechi zote zilizopita, na matatizo yote tuliyonayo na aina ya wachezaji waliopo – hatukutaka Lindelof acheze eneo kubwa na Casemiro ni aina ya wachezaji wanaofurahia kucheza kwa staili hiyo. Nilijaribu kutumia mtindo huo ili kushinda mechi na aina ya wapinzani pia.

"Unapokabia chini unakuwa na uwezo wa kuumiliki mchezo na kisha tuna wachezaji wazuri wa kuhamisha mpira haraka – Garnacho alifanya vizuri sana."

Amorim aliwahi kukiri kwamba amekuwa akimtazama sana kocha wa zamani wa Man United, Mourinho. Jambo hilo lilimfanya apachikwe jina la 'Mourinho 2.0' huko nyuma.

Mourinho, ambaye ni kocha wa Fenerbahce kwa sasa, ametamba sana kwa staili hiyo ya kupaki basi, ambayo imemfanya abebe mataji kwenye timu za Inter Milan na FC Porto alikonyakua Ligi ya Mabingwa Ulaya na Chelsea alikobeba mataji kibao ya Ligi Kuu England.


TAKWIMU ZA MECHI MAN UTD v ARSENAL

-Mashuti golini: Man Utd 6, Arsenal 6

-Mashuti yote: Man Utd 10, Arsenal 16

-Mashuti yaliyozuiwa: Man Utd 2, Arsenal 5

-Umiliki mpira: Man Utd 32%, Arsenal 68%

-Pasi zote: Man Utd 271, Arsenal 585

-Pasi sahihi: Man Utd 204, Arsenal 524

-Kupiga takolin: Man Utd 28, Arsenal 13

-Kucheza faulo: Man Utd 8, Arsenal 11

-Kupiga kona: Man Utd 2, Arsenal 9